
NA; Mwandsihi Wetu – Chato
Wataalamu kutoka katika Sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP ) inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu wamekutana Mjini Chato Mkoani Geita tarehe 8 Juni 2026 kwa lengo la kufanyia mapitio mpango kazi wa Programu hiyo.
Akizungumza katika ufunguzi wa kikao kazi hicho, Mhandisi Enock Nyanda, Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Sekta za Uchumi na Uzalishaji Idara ya Tawala za Mikoa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI alisema lengo la wataalam hao kukutana ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya kikao cha Mawaziri kilichofanyika mapema mwezi Mei mwaka huu.
Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine kiliwataka wataamu hao kufanya mapitio ya kiutendaji katika mpango kazi wa utekelezaj wa Programu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha na kujadili kazi, mapitio ya bajeti sambamba na kufanya tathmini fupi ya kila utekelezaji wa Programu.

Aidha timu hiyo ya wataalam pia itaandaa shughuli zitakazotekelezwa na program kwa mwaka 2027 ilikuweza kufikia malengo pamoja na kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mradi ya Rubambagwe Wilayani Chato pamoja na Kilimi Wilayani Nzega Mkoani Tabora.

Sekta zinazotekeleza Progreamu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) ni Pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo, Shirika la Uvuvi nchini TAFICO, Shirika la Uvuvi Zanzibar ZAFICO, Wizara ya uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Wakala wa Mbegu Nchini ASA, Taasisi ya Uthibiti wa Ubora wa Mbengu Nchini TOSCI na Taasisi ya utafiti wa Mbegu za Kilimo Nchini TARI

.jpeg)
.jpeg)
EmoticonEmoticon