TANZANIA NA KENYA ZASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO SEKTA YA NISHATI

May 05, 2026


 📌*Ni kupitia mauziano ya umeme na upembuzi yakinifu mradi wa Bomba la Gesi Dar-es-Salaam- Mombasa*


Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi na Waziri wa Nishati na Petroli wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Opiyo Wandayi wamesaini makubaliano ya ushirikiano ya kuanza mauziano ya umeme baina ya Tanzania na Kenya pamoja na upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa.

Makubaliano hayo yamefanyika Mei 04, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Samoei Ruto ambaye yuko nchini kwa ziara yake ya kitaifa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »