Na Oscar Assenga,TANGA
MKURUGENZI wa Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani Segule Segule amewataka wamiliki wa visima vya maji katika Wilaya ya Tanga wamepewa siku saba kuhakikisha wanalipia leseni za matumizi ya maji ya chini ya ardhi, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kauli hiyo ameitoa baada ya ukaguzi maalum kubaini kuwepo kwa wamiliki wengi wa visima wanaotumia maji bila kuwa na leseni halali, hali inayosababisha upotevu wa mapato ya Serikali.
Ukaguzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Green Cities unaofadhiliwa na GIZ, unaolenga kutambua visima vilivyopo, ubora wa maji pamoja na kiasi cha maji kinachopatikana. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani, Halmashauri ya Jiji la Tanga na Tanga UWASA.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Segule amesema baadhi ya wamiliki wa visima wamekuwa wakichanganya kati ya leseni ya uchimbaji na ile ya matumizi, akisisitiza kuwa sheria inahitaji kila mmiliki kulipia leseni ya matumizi kila mwaka.
“Kuna watu wanadhani wakishapata leseni ya kuchimba visima wanakuwa wamemaliza kila kitu. Siyo kweli. Sheria inawataka kulipia leseni ya matumizi kila mwaka kwa shilingi 300,000. Tumewapa elimu na sasa tumewapa siku saba—wasipotekeleza, hatua zitachukuliwa,” amesema Segule kwa msisitizo.
Katika zoezi hilo, timu ya wataalamu iliyojumuisha wahandisi, wataalamu wa maabara na maafisa wa serikali za mitaa ilifanya ukaguzi wa kina wa visima katika maeneo mbalimbali, ikiwemo shule, zahanati, vituo vya afya, nyumba za ibada, makazi binafsi na maeneo ya shughuli za kiuchumi kama viwanda na ufyatua matofali.
Kwa upande wao, baadhi ya wamiliki wa visima wameonyesha utayari wa kufuata maelekezo hayo, wakikiri umuhimu wa maji hayo katika shughuli zao za kila siku.
“Tutakwenda ofisini kesho kufuata utaratibu wa kulipia leseni. Maji haya yanatusaidia sana katika kazi zetu za kufyatua matofali,” amesema Joseph Samwel wa Katemi Enterprises.
Naye Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Saruji, Fahad Salumu, amesema tathmini hiyo imewasaidia kupata picha halisi ya idadi ya visima vilivyopo pamoja na ubora wa maji katika eneo lake.
Wakati huohuo, Mkaguzi wa ubora wa maji kutoka maabara ya Bodi hiyo, Mpajieli Joseph, amesema tayari sampuli 30 za maji zimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kina zaidi.
Akitoa mfano wa matokeo ya awali, mtaalamu wa maji ya chini ya ardhi, Nice Ninja, amesema vipimo vya mwanzo katika Shule ya Sekondari Maweni vinaonyesha maji hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu, ikiwemo kunywa, huku uchunguzi zaidi ukiendelea maabara kuu.
Hata hivyo, Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani imesema taarifa kamili ya tathmini hiyo itatolewa mara baada ya kukamilika kwa mradi wa Green Cities.
Wamiliki wa visima vya maji katika Wilaya ya Tanga wamepewa siku saba kuhakikisha wanalipia leseni za matumizi ya maji ya chini ya ardhi, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Onyo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani, Segule Segule, baada ya ukaguzi maalum kubaini kuwepo kwa wamiliki wengi wa visima wanaotumia maji bila kuwa na leseni halali, hali inayosababisha upotevu wa mapato ya Serikali.
Ukaguzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Green Cities unaofadhiliwa na GIZ, unaolenga kutambua visima vilivyopo, ubora wa maji pamoja na kiasi cha maji kinachopatikana. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani, Halmashauri ya Jiji la Tanga na Tanga UWASA.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Segule amesema baadhi ya wamiliki wa visima wamekuwa wakichanganya kati ya leseni ya uchimbaji na ile ya matumizi, akisisitiza kuwa sheria inahitaji kila mmiliki kulipia leseni ya matumizi kila mwaka.
“Kuna watu wanadhani wakishapata leseni ya kuchimba visima wanakuwa wamemaliza kila kitu. Siyo kweli. Sheria inawataka kulipia leseni ya matumizi kila mwaka kwa shilingi 300,000. Tumewapa elimu na sasa tumewapa siku saba—wasipotekeleza, hatua zitachukuliwa,” amesema Segule kwa msisitizo.
Katika zoezi hilo, timu ya wataalamu iliyojumuisha wahandisi, wataalamu wa maabara na maafisa wa serikali za mitaa ilifanya ukaguzi wa kina wa visima katika maeneo mbalimbali, ikiwemo shule, zahanati, vituo vya afya, nyumba za ibada, makazi binafsi na maeneo ya shughuli za kiuchumi kama viwanda na ufyatua matofali.
Kwa upande wao, baadhi ya wamiliki wa visima wameonyesha utayari wa kufuata maelekezo hayo, wakikiri umuhimu wa maji hayo katika shughuli zao za kila siku.
“Tutakwenda ofisini kesho kufuata utaratibu wa kulipia leseni. Maji haya yanatusaidia sana katika kazi zetu za kufyatua matofali,” amesema Joseph Samwel wa Katemi Enterprises.
Naye Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Saruji, Fahad Salumu, amesema tathmini hiyo imewasaidia kupata picha halisi ya idadi ya visima vilivyopo pamoja na ubora wa maji katika eneo lake.
Wakati huohuo, Mkaguzi wa ubora wa maji kutoka maabara ya Bodi hiyo, Mpajieli Joseph, amesema tayari sampuli 30 za maji zimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kina zaidi.
Akitoa mfano wa matokeo ya awali, mtaalamu wa maji ya chini ya ardhi, Nice Ninja, amesema vipimo vya mwanzo katika Shule ya Sekondari Maweni vinaonyesha maji hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu, ikiwemo kunywa, huku uchunguzi zaidi ukiendelea maabara kuu.
Hata hivyo, Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani imesema taarifa kamili ya tathmini hiyo itatolewa mara baada ya kukamilika kwa mradi wa Green Cities.

.jpg)

.jpg)
EmoticonEmoticon