BODI MPYA TFS YAANZA KAZI RASMI, YAPOKEA MPANGO WA BIASHARA 2026/2027

April 02, 2026


Morogoro

Bodi ya Tano ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanza rasmi majukumu yake kwa kufanya kikao cha 47 cha Bodi, ambacho pia ni kikao cha kwanza cha bodi hiyo mpya.

Kikao hicho kimefunguliwa leo Aprili 2, 2026 mkoani Morogoro na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Luteni Mstaafu Chiku Abdallah Sumbu Gallawa, katika Ukumbi wa Kituo cha Mbegu Bora za Miche ya Miti cha TFS.

Kabla ya kikao hicho, wajumbe walifanya vikao vya kamati kuanzia Machi 31 hadi Aprili 1, 2026, kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji ya wakala.

Pamoja na mambo mengine, Bodi ilipokea na kujadili Mpango wa Biashara wa TFS kwa mwaka wa fedha 2026/2027, sambamba na taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya taasisi.

Kuanza kwa kikao hicho kunafuatia uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanywa Februari 13, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji.











Share this

Related Posts

Previous
Next Post »