Wanawake watumishi wa Mamlaka Hifadhi ya Ngorongoro katika muendelezo wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, wamedhihirisha kwamba mchawi wa mwanamke si mwanamke kwa kutembelea shule ya Sekondari ya wasichana Ngorongoro na kuwapa tabasamu la msaada wa vifaa mbalimbali
Akiongea kwa Niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Afisa Uhifadhi Mkuu Sarah Lushu ameeleza kuwa vitu ambavyo Mamlaka vinajumuisha vyakula, Sabuni, vifaa vya kujifunzia, taulo la kike, Vyombo vya kuogea, kupikia na kufulia na mahitaji mbalimbali mahususi kwa wanafunzi wanawake ilo kuwaongezea tabasabu na kuonyesha nguvu ya mwanamke katika Jamii.
"Msaada huu ni sehemu ya jitihada za Shirika kupitia kamishna wa Uhifadhi kuimarisha uhusiano na jamii iliyopo ndani ya Hifadhi na kuhakikisha kuwa wanafunzi hasa wa kike wanapata mahitaji muhimu ya kuwapa utulivu wa kusoma na kupata ufaulu mzuri" alifafanua PCO Sarah.
Msaada huu unadhihirisha wazi kuwa wanawake ni watu wa kusaidiana na mchawi wa mwanamke sio Mwanamke.





EmoticonEmoticon