Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amefungua rasmi kituo kipya VIP Sober House Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Tanzania kukabiliana na uraibu wa dawa za kulevya na pombe.
PILIMISSANAH FOUNDATION (PIMIFO) ni kituo ambacho kinatoa huduma za urekebishaji kwa watu wanaosumbuliwa na uraibu kwa zaidi ya miaka 14 sasa.
Lyimo alisema juhudi za Wadau binafsi ni muhimu katika kukabiliana na uraibu, ambao ni tatizo linaloendelea kuathiri afya na maendeleo ya jamii. "Uraibu wa dawa za kurevya na pombe limeathili familia nyingi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Vituo kama hivi vimekua vikipatikana nje ya nchi, sasa Tanzania imebahatika kupata huduma hii hapa hapa nchini," alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa PIMIFO, Pilli Missanah,alisema kituo hicho kinatoa huduma kwa heshima, faragha, na ubora. "Watu wengi walikosa huduma kwa kuogopa unyanyapaa na kukosa faragha. Kituo hiki kinatoa nafasi salama kwa ajili ya kupona," alisema.
Kituo hicho kina sehemu za mazoezi, ushauri nasaha, burudani, na lishe bora. Msanii wa Bongo Flavour, Abdulrahman Kasembe aka Dulayo, ameanza kupata matibabu huko, alisema "nashukuru kupata fursa ya kujenga maisha yangu tena upya na kurudia katika muziki nikiwa vizuri".
Uraibu wa dawa na pombe ni changamoto kubwa Tanzania na duniani kote kutokana na ukosefu wa ajira, utandawazi na mmomonyoko wa maadili, dawa za kulevya na unywaji wa pombe ulio kithiri.
Serikali imedumisha kampeni za uelewa na ushirikiano na mashirika binafsi na ya kidini katika kutoa huduma za urekebishaji.
Sasa kituo kinaendelea kupokea waraibu nchini na Kanda nzima ya Africa Mashriki.Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amefungua rasmi kituo kipya VIP Sober House Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Tanzania kukabiliana na uraibu wa dawa za kulevya na pombe.
PILIMISSANAH FOUNDATION (PIMIFO) ni kituo ambacho kinatoa huduma za urekebishaji kwa watu wanaosumbuliwa na uraibu kwa zaidi ya miaka 14 sasa.
Lyimo alisema juhudi za Wadau binafsi ni muhimu katika kukabiliana na uraibu, ambao ni tatizo linaloendelea kuathiri afya na maendeleo ya jamii. "Uraibu wa dawa za kurevya na pombe limeathili familia nyingi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Vituo kama hivi vimekua vikipatikana nje ya nchi, sasa Tanzania imebahatika kupata huduma hii hapa hapa nchini," alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa PIMIFO, Pilli Missanah,alisema kituo hicho kinatoa huduma kwa heshima, faragha, na ubora. "Watu wengi walikosa huduma kwa kuogopa unyanyapaa na kukosa faragha. Kituo hiki kinatoa nafasi salama kwa ajili ya kupona," alisema.
Kituo hicho kina sehemu za mazoezi, ushauri nasaha, burudani, na lishe bora. Msanii wa Bongo Flavour, Abdulrahman Kasembe aka Dulayo, ameanza kupata matibabu huko, alisema "nashukuru kupata fursa ya kujenga maisha yangu tena upya na kurudia katika muziki nikiwa vizuri".
Uraibu wa dawa na pombe ni changamoto kubwa Tanzania na duniani kote kutokana na ukosefu wa ajira, utandawazi na mmomonyoko wa maadili, dawa za kulevya na unywaji wa pombe ulio kithiri.
Serikali imedumisha kampeni za uelewa na ushirikiano na mashirika binafsi na ya kidini katika kutoa huduma za urekebishaji.
Sasa kituo kinaendelea kupokea waraibu nchini na Kanda nzima ya Africa Mashriki.

EmoticonEmoticon