MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR ASEMA KUNA UMUHIMU VIJANA WAFUNDISHWE HISTORIA YA CCM

February 05, 2026



Na Oscar Assenga, MUHEZA


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema wakati chama cha Mapinduzi (CCM) kinaadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwake kuna umuhimu mkubwa vijana wafundishwe historia yake na waijue ikiwemo misingi ya uwepo wake.

Abdulla ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM aliyasema hayo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika kimkoa Stendi ya Bombani mjini Muheza.

Alisema kwamba wakijua msingi wa kuwepo chama hicho na wakitembea watatembea na maono mazuri mno lakini wasipojua bado kuna kitu watakuwa wanawanyima hivyo lazima wajue kwanini TANU na ASP ziliungana.


Aidha alisema pia wajue pia viliingana kwa malengo gani na wafahamu kwanini kuna chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndio chama cha wanyonge hata ukiangalia vijiji vyote Tanzania kila mahali, kata utakuta kuna mradi kama hakuna shule utakuta mradi wa zahanati,barabarani,mradi wa maji na miradi mengine mbalimbali kwa sababu ya kujali maslahi ya wananchi wa Tanzania.



Alisema pia Rais Dkt Samia Suluhu ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho amefanya mambo mengi makubwa na mazuri hivyo wana kila sababu ya kumuenzi na kumtunza ili aweze kuwafanyia mambo mengi na makubwa zaidi.



Alieleza kwamba Rais Dkt Samia katika kipindi cha miaka mitano amefanya mambo makubwa na ahaidi yake miaka mitano hii amehaidi mambo mengi mazuri hivyo wampe ushirikiano ili aweze kutekeleza yale yote aliyohaidi.



Abdulla alisema kwamba CCM ndio chama pekee ambacho kinadumisha muungano wetu kwa Tanganyika na Zanzibar vyama vyengine vinavisikia vikisema tu kwenye kampeni zao wao jambo la kwanza wakipata wanavunja muungano jambo ambalo halina afya kwa ustawi wa maendeleo hapa nchini.



Hata hivyo alisema kwamba hivi sasa watanzania wanahitaji mambo mawili makubwa ambayo ni amani na maendeleo ambayo ndio tunu kubwa ya mafanikio katika jambo lolote lile.



“Leo hii mmeona zile changamoto zilizojitokeza baadhi ya mikoa Octoba 29 ya kutetereka kwa amani kila mmoja hana furaha unatafuta taarifa haupati,hakuna nyumba ya mtanzania inayokosa simu hivyo akikosa kupata habari hivyo kupitia maadhimisho haya wachukue wale wenye mawazo tofauti kuwashawishi watanzania kufanya mambo yasiyokuwa na tija kwa nchi”



Hata hivyo alisema kwamba watanzania wana mahitaji mawili ya amani na maendeleo ukikamilisha hayo umekamilisha kazi na hayo huwezi kuyapata popote zaidi ya CCM.



Pongezi.



Mlezi huyo wa CCM aliwapongeza wananchi wa Tanga kutokana na kudumisha amani Octoba 29 na hivyo kufanya uchaguzi kwa amani na hatimaye uchaguzi ulifanyika kwa hali ya utulivu.



Alisema kwamba kwamba hali ya amani inayozungumzwa haiwasaidii wana CCM pekee bali inasaidia wananchi wote wa Tanzania na hata wasiokuwa watanzania waliopo nchini kwa shughuli zao za maendeleo na njia moja ya kuwekeza sehemu yoyote duniani jambo la kwanza wanaangalia amani wakiona ipo ndio wanaendelea na hatua nyengine.


“Leo tunapoadimisha miaka 49 ya kuzaliwa CCM chama ambacho kinaendelea kuaminiwa na watanzania zaidi ya milioni 60 na ni matumaini yangu watanzania tutaendelea kukikiamini CCM kwa kazi nzuri inayofanyika”Alisema



“Kwa mkoa wa Tanga maendeleo makubwa yanaonekana tumeona Bandari ya Tanga zaidi ya Bilioni 429 Dkt Samia Suluhu ameziweka pale na mkapeleka maombi ya uwanja wa Ndege ambayo Serikali itaanza kuyafanyia kazi”Alisema



Hata hivyo alisema kuna ujenzi wa miradi mbalimbali inaendelea ikiwemo Barabara ya Handeni -Kibirashi- kilindi na inaunganisha na Singida zipo taarifa nje za barabara hizo ameitaja kwa sababu ya kuunganisha na mikoa mingine na Bandari.



Alisema kwamba maana yake barabara ikikamilika wale wote wanaoleta mizigo kutoka nchi jirani watatumia Bandari ya Tanga na ipo miradi mingi inaendelea na ahadi ya CCM ni kumaliza changamoto za wananchi.



Mwisho,



















Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »