BALOZI DKT.MIGIRO IBADANI KUMUAGA JENISTA MHAGAMA

December 13, 2025

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa CCM, amejumuika na waombolezaji wengine kushiriki ibada ya kumuaga aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, marehemu Jenista Joakimu Mhagama, inayofanyika katika Kanisa Katoliki Kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawaongoza waombolezaji katika shughuli hiyo ya kumuaga marehemu Jenista Mhagama, kanisani hapo.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »