REA YANG'ARA MAONESHO YA WIKI YA CHAKULA TANGA

October 16, 2025


*📌Waziri Mkuu aitunuku REA tuzo ya pongezi kwa uhamasishaji wa matumizi nishati safi*


*📌Majiko ya gesi 500 yauzwa kwa bei ya ruzuku kwenye maonesho*


*📌Asisitiza kulinda mazingira na kuacha ukataji wa miti hovyo*


📍Tanga


Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hapa nchini.



Katika hatua nyingine, Mhe. Majaliwa ameipatia tuzo ya pongezi REA ambapo imeibuka kuwa mshindi wa pili wa banda bora katika kuhudumia wananchi katika maadhimisho ya Wiki ya Chakula yaliyofanyika mkoani humo.

Naye, Mhandisi kutoka REA, Ramadhan Mganga amesema Rais Samia ni kinara wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati zisizo safi na salama na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa REA mkoani Tanga, Mha. Raphael Njango ameeleza kuwa, utekelezaji wa miradi ya REA katika mkoa huo inaendelea ambapo vitongoji 2,382 vimefikiwa na huduma ya umeme sawa na asilimia 52.6 ya vitongoji vyote 4,531.



Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeshiriki katika maadhimisho hayo ambapo imeuza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya shilingi 17,500 tu ambapo jumla ya majiko 500 yameuzwa mkoani humo kupitia maonesho hayo.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »