WAZIRI MKUU AIPONGEZA WIZARA YA NISHATI KWA USIMAMIZI THABITI WA MIRADI

October 16, 2025


📌 *Ni wakati akifunga Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani*


📌 *Asema usimamizi thabiti wa miradi unapelekea wananchi kupata huduma bora*


📍Tanga


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim  Majaliwa amepongeza Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa utekelezaji na usimamizi miradi mbalimbali ya nishati nchini.

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo jijini Tanga  wakati akifunga Maadhimisho  ya Kitaifa ya  Siku ya Chakula ya Duniani ambayo leo  yamefikia kilele chake.


Mhe. Majaliwa amesema kuwa usimamizi mzuri wa miradi ya Nishati umepelekea wananchi kuendelea kupata huduma bora.

Katika maadhimisho hayo ya Siku ya Chakula Duniani  yaliyoanza  tarehe 10 Oktoba 2025 yamepelekea wananchi kupata elimu kuhusu mafanikio ya sekta ya nishati na miradi inayoendelea huku  wananchi 500 wakinufaika na mitungi ya gesi iliyokuwa ikiuzwa kwa bei ya Ruzuku ya shilingi 17,500/=.

Katika hatua nyingine,  Waziri Mkuu amekabidhi tuzo kwa Wakala wa  Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni kupongeza juhudi za taasisi hiyo kupitia maadhimisho hayo ya Siku ya Chakula Duniani.




#NishatiTupokazini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »