WAKURUGENZI WA RASILIMALIWATU KUHAKIKI RASIMU YA KANUNI ZA KUDUMU KATIKA UTUMISHI WA UMMA

October 02, 2025

Mwakilishi wa Katibu Mkuu ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi wakati akifungua kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Sehemu ya Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi wakiwa katika kikao kazi kilichoandaliwa na Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa lengo la kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.



Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus Kapinga akifuatilia maoni mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa wakati wa kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa kikao kazi hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Michael John.



Sehemu ya Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi wakiwa katika kikao kazi kilichoandaliwa na Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa lengo la kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.



Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Prisca Lwangili akiwasilisha maoni yake wakati wa kikao kazi cha kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.



Afisa Rasilimaliwatu Mwandamizi, Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Anne Yusuph akiwasilisha Rasimu ya Mapendekezo ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 wakati wa kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu hiyo kilichofanyika jijini Dodoma



Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia kikao kazi cha kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Sehemu ya Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Mishahara na Marupurupu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Gubas Vyagusa (aliyesimama) akiwasilisha maoni yake wakati wa kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mhasibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Tumwimbilege Ilomo akifuatilia kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Wengine ni Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi

Sehemu ya Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia kikao kazi cha kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Wengine ni Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi

Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi mara baada ya kufungua kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (katikati mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi mara baada ya kufungua kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mkaguzi wa Ndani, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Martha Wililo (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, Ukimwi na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Mwanaamani Mtoo (kulia) wakifuatilia maoni kutoka kwa Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kutoka katika Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, na Taasisi wakati wa kikao kazi kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.


Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma


Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi amesema Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) ni nyenzo muhimu katika Usimamizi wa Utawala na Rasilimaliwatu ndani ya taasisi za Umma.

SACP. Mahumi amesema hayo, wakati akifungua kikao kazi cha wadau kilicholenga kuhakiki Rasimu ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma Toleo la Nne la Mwaka 2025 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

SACP. Mahumi amesema, kupitia Sera ya Menejimenti na Ajira, Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Kanuni zake za 2022 pamoja na miongozo ya Kiutumishi inayotolewa na Serikali ni vitendea kazi muhimuvinavyotumika kusimamia Utumishi wa Umma ili kuwa na ufanisi.

Kupitia kikao kazi hicho SACP. Mahumi amewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Utumishi kuona namna ya kutoa maoni na ushauri ili kuboresha zaidi Sera na Kanuni zinazotakiwa kufanyiwa mabadiliko.

Kadhalika, SACP. Mahumi amesema, mabadiliko ya Sera na Kanuni mbalimbali katika Utumishi wa Umma, pia zimeleta mabadiliko katika eneo la Upimaji wa Utendaji kazi ambao awali ulikuwa unajulikana kama (OPRAS) ambayo kwa sasa unajulikama kwa jina la PEPMIS, mabadiliko ya Sheria ya Utumishi wa Umma pamoja na Nyaraka mbalimbali ambazo zinatoa maelekezo tofauti na ya awali ambayo yalikuwa yakifanyiwa kazi.


Akihitimisha hotuba yake, SACP. Mahumi amesema, matokeo ya kikao kazi hicho yalenge katika kutoa mwelekeo chanya wa nyaraka sahihi kupitia Sera na Kanuni zitakazoboreshwa.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »