MAMIA ya Wananchi wa Kata ya Mwandoya ndani ya Jimbo la Kisesa,wilayani Meatu wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi wakati akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara leo Septemba 2,2025,wakati akiendelea na Mikutano yake ya Kampeni mkoani Simiyu.
Katika mkutano huo wa kampeni,Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi alimnadi Mbunge wa Jimbo hilo la Kisesa,Musa Godfrey Mbuga pamoja na diwani wa kata ya Lubiga,Juma Mpina ambaye ni kaka wa mbunge wa zamani wa jimbo laKisesa, Luaga Mpina
Pamoja na mambo mengine Balozi Dkt.Emmeanuel Nchimbi amekuwa akiinadi Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia Suluhu,Mgombea mwenza wa Urais,wabunge na madiwani wa Chama hicho.
EmoticonEmoticon