Na Oscar Assenga,TANGA
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh.Milioni 10,500,000 kutokana na ufuatiliaji utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya Barabara mkoani hapa.
Akizungumza leo na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha Aprili hadi June 2025 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga Ramadhani Ndwatah ambapo alisema kwamba katika jitihada za kuzuia vitendo vya rushwa taasisi hiyo inalo jukumu la kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendelelo.
Alisema wanafanya hivyo ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi ili kufikia malengo ya Serikali ya upelekaji wa miradi hiyo kwa wananchi ambapo katika kutekeleza hilo walifuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo 29 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 7 katika sekta ya elimu na barabara na kubaini.
Mkuu huyo wa Takukuru alisema kwamba walibaini Sh.Milioni 475 zilitolewa kwa Halmashauri ya wilaya ya Muheza kupitia fedha za Mfuko wa Barabara kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa mita 800 ambapo katika ufuatiliaji ilibainika kwamba kwa mujibu wa ramani na makadirio ya ujenzi (BOQ) barabara hiyo ilitakiwa kuwa na nguzo za taa za umeme jua zipatazo 29 lakini zilizowekwa ni nguzo za taa 26 .
Aidha alisema kwamba baada ya kubaini mapungufu hayo Takukuru ilichukua hatua mbalimbali ikiwemo kufanya mawasiliano na wahusika ambao ni ofisi ya Tarura wilaya na kuwaeleza mapungufu yaliyobainika.
Hata hivyo alisema kwamba mapendekezo ya maboresho na marekebisho yametekelezwa kwa kuwekwa nguzo na taa zake 3 zenye thamani ya Sh.Milioni 10,500,000.00 zilizkuwa na ubora uliokusudiwa
Mkuu huyo wa Takukuru alisema kwamba pia miradi 10 yenye thamani ya Bilioni 2,869,191,531.00 ilibainika kuwa na mapungufu kama vile miradi kutekelezwa bila malipo ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ,miradi kutokuzingatia michoro na ramani,miradi kutekelezwa kwa muda mrefu zaidi ya muda uliowekwa kwenye mkataba,kitabu cha kutoa na kupokea vifaa (Issue Voucher) kutokujaza kwa wakati.
Aliongeza kwamba kutokana na uwepo wa mapungufu hayo hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuyarekebisha ikiwemo kuzijulisha mamlaka husika.
EmoticonEmoticon