Na John Mapepele
Mgombea wa Nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Rufiji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)na MNEC kupitia Mkoa wa Pwani, Ndugu Mohamed Omary Mchengerwa amewaongoza maelefu ya wanaCCM wa Mkoa wa Pwani kuhudhuria uzinduzi wakihistoria wa kampeni ya mgombea wa urais kwa CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, uzinduzi huu imepambwa na wasanii mbalimbali ambao wameburidisha umati wa maelfu ya wananchi waliohudhuria.
Mhe. Mchengerwa maarufu kwa jina la Mchengerwa Mtu Kazi ( MMK) anaingia kwenye kinyang'anyiro cha kutetea kiti chake cha ubunge baada ya kuliongoza jimbo hilo kwa mafanikio makubwa.
Pia katika sekta ya Afya kumekuwa na ongezeko la zahanati, vituo vya afya na hospitali.
Katika zoezi la kura za kusaka mgombea ubunge wa CCM kwa jimbo la Rufiji mwaka huu ambao ulikuwa na wagombea wanne wa nafasi hiyo Mhe. Mchengerwa aliweza kushinda kwa zaidi ya asilimia 99 ya kura zote zilizopigwa.
EmoticonEmoticon