Aliyekuwa mbunge wa Tanga Mjini, Ummy Mwalimu leo Agosti 25, 2025 amewataka wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Tanga kuacha makundi na kujikita katika kutafuta kura za ushindi wa kishindo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassani ambaye ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mauungano wa Tanzania kupitia CCM pamoja na kumuunga mkono mgombea ubunge wa jimbo la Tanga mjini ndugu. Kassim Mbaraka Amali na kukiwezesha Chama hicho kushinda katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 29 Octoba 2025.
“Watu wa Tanga tunakila sababu za kumpa kura zote za ndio Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri alizofanya Tanga mjini na Taifa letu, hivyo nawaomba sana wanatanga twendeni tukamlipe hisani Dkt. Samia na kazi yetu iwe ni kutafuta ushindi wa Chama Cha Mapinduzi”
EmoticonEmoticon