KAILIMA AFUNGA KIKAO CHA UPANGAJI WA RATIBA YA KAMPENI ZA WAGOMBEA URAIS

August 26, 2025

 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu Kailima R.K, amefunga kikao cha siku mbili cha Tume na Vyama vya Siasa 18 vyenye usajili kamili na ambavyo vimependekeza wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania  na Makamu wa Rais, kwa lengo la kujadili na kupanga kwa pamoja ratiba ya kampeni za vyama hivyo. 

Kikao hicho kilichoketi Agosti 25 na 26, 2025  kilishirikisha vyama vya Civic United Front (CUF), National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi), Union for Multiparty Democracy (UMD), Chama cha Mapinduzi (CCM), National League for Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party (UPDP) na National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic Alliance Party (ADA-TADEA).
 
Vyama vingine ni Tanzania Labour Party (TLP), United Democratic Party (UDP), Madini Kilimo Nishati (MAKINI), Democratic Party (DP), Sauti ya Umma (SAU), Alliance for African Farmers Party (AAFP), Chama cha Kijamii (CCK), Alliance for Democratic Change (ADC),Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo).

Kampeni za Uchaguzi zinatarajiwa kuanza Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 28, 2025 nchini kote ambapo wagombea watakaoteuliwa na Tume watafanya kampeni za kunadi sera za vyama vyao kutafuta ridhaa ya wananchi kuwapigia kura Oktoba 29, 2025 katika uchaguzi mkuu.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »