DC KILWA AFANYA ZIARA SONGOSONGO, APONGEZA TPDC KWA MIRADI YA KIJAMII

August 14, 2025
Agosti 13, 2025

Songosongo, Lindi – Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Abdallah Nyundo, amefanya ziara ya kutembelea miundombinu ya bomba la gesi asilia iliyopo kisiwaniSongosongo, Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi, kwa lengo la kujionea maendeleo nauwekezaji wa miundombinu hiyo muhimu kwa uchumi wa taifa.

Katika ziara hiyo, Mhe. Nyundo aliambatana na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalamaya Wilaya, ambapo walipata maelezo ya kina kuhusu hali na uendeshaji wa miundombinu yagesi asilia.

Akitoa ufafanuzi wa maendelo ya Kiwanda kwa Mkuu wa Wilaya , Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Songosongo, Mhandisi James Mwaipasi, alisema kiwanda kinaendeleakufanya kazi kwa ufanisi kwa kuendana na viwango vya kimataifa vya uzalishaji na usalamawa mazingira.

“Kiwanda cha Songosongo kinaendelea kuzalisha gesi kwa kiwango cha juu cha ubora, hukutukizingatia viwango vya kimataifa vya usalama na uendelevu wa mazingira.,” alisemaMhandisi Mwaipasi

Sambamba na ziara hiyo, Mhe. Nyundo alipata fursa ya kuzungumza na wananchi waSongosongo kupitia mkutano wa hadhara, ambapo alisisitiza umuhimu wa kulindamiundombinu ya bomba la gesi na kuwataka kuendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleoya Petroli Tanzania (TPDC) katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa rasilimali hiyo.

“Miundombinu ya gesi ni mali ya Watanzania wote. Ni jukumu letu kuhakikisha inalindwadhidi ya uharibifu wowote. Ushirikiano wenu na TPDC ni nguzo muhimu ya kulindauwekezaji huu na kuhakikisha manufaa yake yanaendelea kwa vizazi vijavyo,” alisema Mhe. Nyundo.

Aidha, alilipongeza TPDC kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii kupitia mpangowa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), ikiwemo kuboresha huduma za maji, afya, elimu nakuimarisha utawala bora kisiwani humo.

“Nawapongeza TPDC kwa kazi kubwa mnayoifanya kupitia miradi ya CSR. Mmewezeshawananchi kupata huduma bora zaidi na mnaendelea kuleta maendeleo ya kweli katikajamii,” aliongeza Mhe. Nyundo.

Kwa upande wao, wananchi wa Songosongo walieleza kuridhishwa na juhudi za TPDC katika kuendeleza miradi ya kijamii, hususan mradi wa maji unaoendelea kujengwa.

“Tunashukuru TPDC kwa kukamilisha maradi wa umeme na sasa mindombinu ya umeme niimara na umeme haukatiki tena,. Pia tunashuruku kwa kutuletea mradi wa maji hiiitatuondolea changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama ambayo tumekuwanayo kwa muda mrefu,” alisema Athuman Bakiri.

Ziara hiyo imedhihirisha mshikamano kati ya Serikali, TPDC na jamii katika kulindamiundombinu ya gesi asilia na kuhakikisha wananchi wananufaika moja kwa moja nauwekezaji unaofanyika katika sekta hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Abdallah Nyundo alipotembelea kiwanda cha kuchakata gesi asilia
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Abdallah Nyundo akiwa katika mkutano na wananchi wasongosongo
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »