CDE Mwalimu Nebu Malekela (katikati), wa Shule ya Msingi Magereza iliyopo Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya akikata keki wakati wa sherehe ya kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa aliyo sherehekea na watoto wenye uhitaji wanaolelewa Kituo cha malezi ya watoto hao Hospitali ya Igogwe Mei 12, 2025. Kushoto ni Mlezi wa kituo hicho, Sister Gloria Mwanjelila.
...................................
Na Dotto Mwaibale
JAMII imetakiwa kujenga tabia ya kusaidia watu wenye uhitaji
hasa watoto kwani inasaidia kuwapa faraja na kujiona kama watoto wengine wanaoishi
na familia zao.
Ombi hilo limetolewa na Mlezi wa Kituo cha kulea watoto
wenye uhitaji katika Hospitali ya Igogwe iliyopo Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa
wa Mbeya, Sister Gloria Mwanjelila wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa Cde.
Mwalimu Nebu Malekela wa Shule ya Msingi Magereza Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya iliyofanyika Mei 12, 2025.
“Hawa watoto wanahitaji faraja kama wanayopata watoto
wengine katika familia zao jamii inapokuja kuwatembelea na kushiriki nao kwa
mambo mbalimbali kwao inakuwa faraja kubwa na si lazima mpaka kutoa msaada wa
vitu ingawa ni wa muhimu kulingana na mahitaji yao mbalimbali,” alisema
Mwanjelila.
Akimzungumzia Mwalimu huyo alisema amekuwa ni mtu wa kujitoa mara kwa mara kutembelea kituo hicho na kutoa msaada kwa watoto hao na kueleza kuwa hata wakati wa kusherehekea sikukuu ya pasaka alifika katika kituo hicho na kuwaletea vitu mbalimbali akiwa ameongoza na wanajumbe Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) kutoka Kata ya Kiwira baada ya kuratibu tukio hilo.
“Hawa watoto ni wa jamii nzima na ndio tunaowategemea kuwa
viongozi wa kesho sisi kama walezi wao hatuwezi kuwatoshelezea mahitaji yao
yote hivyo kwa pamoja tukishirikiana tutaweza kuwapatia mahitaji yao mengine
ambayo wanayakosa kutoka kwetu,” alisema mlezi huyo.
Alisema Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanaznia Dkt. Samia Suluhu Hassan haiwezi kuvihudumia vituo vyote vyenye wahitaji
hapa nchini hivyo ni vema jamii ikajenga utamaduni wa kusaidia eneo hilo ikiwa
ni kuungamkono jitihada hizo za Serikali
Akizungumza wakati wa sherehe hiyo Mwalimu Nebu Malekela
alisema aliona sherehe ya kumbukizi yake ya kuzaliwa afike katika kituo hicho
na kusherehekea na watoto hao kwa kukata keki pamoja ambapo pia aliwapelekea
zawadi.
“Lilikuwa tukio dogo lakini lenye furaha tulikata keki , tukala,
kunywa, kuimba na kucheza pamoja na watoto hakika tuli ‘enjoy’sana,” alisema
Mwalimu Malekela.
Ndugu zangu wanajamii
Neno la Mungu linasema dunia na vyote vilivyopo ni mali ya Mungu pamoja na wewe
mwenyewe na hata akiamua kuichukua mali zake atazichukua zote lakini kwa upendo
mkubwa ametupa akili ya kuimiliki mali hiyo na zaidi ya yote akatupa nafasi ya
kumrudishia sehemu ndogo tu ya mali zetu akituhitaji kuwasaidia wahitaji badala
yake na ndio maana anatoa nafasi kwa wenye kitu kidogo kulisaidia kundi hilo
kwani kutoa ni moyo na wala sio utajiri.
Mwalimu Nebu Malekela akionesha upendo kwa kumlisha keki mmoja wa watoto wa kituo hicho
Mwalimu Nebu Malekela akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao wenye uhitaji
EmoticonEmoticon