WANANCHI wanaofanya shughuli za Uvuvi na Wakulima wa Zao la Mwani wanaoishi katika kijiji cha Mwaboza wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga wameishukuru taasisi ya Umoja wa wasaidizi wa Sheria 'UWASHEM' kwa kuwawezesha kutatua mgogoro baina yao kutokana na matumizi ya rasilimali bahari ambapo kupitia elimu waliyoipata imewawezesha kuwaunganisha.
Awali wakizungumza katika mdahalo wa pamoja ulioandaliwa na taasisi hiyo kwa lengo la kutambua changamoto zilizopo baina yao Kila mmoja ameonekana kumshutumu mwingine kuwa chanzo cha mgogoro kwa kile walichoeleza kuwa wamekuwa wakigombania maeneo hali iliyopelekea kukosa maelewano na hatimaye kuwaingiza kwenye mgogoro.
Wakizungumza baadhi yao wamesema kuwa pamoja na elimu waliyoipata kupitia shirika la UWASHEM' ni vyema Serikali ikatenga maeneo maalum ili kuwasaidia wananchi hao kufanya shughuli zao bila bughuza na hatimaye kuendelea kujipatia kipato Chao cha Kila siku
Mratibu wa miradi kutoka shirika la UWASHEM' Swalehe Sokolo amesema kuwa kupitia mradi huo wanaoutekeleza imesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto baina ya Wavuvi na Wakulima wa Zao la Mwani ambapo pia wameweza kuwaunganisha na viongozi wa Serikali.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa KUJENGA AMANI PAMOJA kutoka shirika la shirika la We World Zacharia Msabila amesema wanafanya kazi na taasisi zilizopo karibu na jamii ambapo kupitia ufadhili wanaoutoa itasaidia kufikia malengo waliyoyatarajia.
Diwani wa kata ya Moa Staruki Njama amekiri uwepo wa migogoro ya muda mrefu biana ya Wakulima wa Zao la Mwani na Wavuvi katika kijiji cha Mwaboza ambapo shirika la UWASHEM' limekuja kuleta suluhisho kupitia elimu waliyoitoa ambapo amewapongeza kwa jitihada walizozifanya huku akisisitiza wananchi kuendelea kufuatia na kutekeleza Sheria zilizowekwa.
Shirika la umoja wa usaidizi wa Sheria Mkinga "UWASHEM'' linatekeleza mradi wa KUJENGA AMANI PAMOJA katika wilaya hiyo kwa kushirikiana na shirika la 4H Tanzania ukifadhiliwa na shirika la We World kwa lengo la kuleta amani baina ya wananchi kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kupelekea uvunjifu wa amani.
EmoticonEmoticon