WAKULIMA WA MWANI, WAVUVI MKINGA WALISHUKURU SHIRIKA LA TAWSEI KUWAPATIA ELIMU

April 07, 2025




Na Oscar Assenga, MKINGA



WAKULIMA wa Kilimo cha Mwani na Wavuvi kata ya Manza na Mayomboni wilayani Mkinga Mkoani Tanga wamelishukuru Shirika la Tanzania Women For Self Initiatives (TAWSEI) kwa kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa Amani  wakati wa utekelezaji wa shughuli zao kutokana na mgogoro baina yao

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa kata ya Mayomboni wilayani kupitia mradi wa  Amani ni Tunu ambao ulitokana na mradi mkubwa wa "Kujenga Amani Pamoja "kupitia warsha zilizofanyika kwa kushirikiana na Shirika la 4 H Tanzania,We Word na Taswei kupitia ufadhili wa Umoja wa Mataifa ya Ulaya.

Ambapo kulibainika mgogoro mkubwa baina ya wakulima wa Mwani na Wavuvi kutokana na shughuli zao kufanyika katika moja la bahari ya Hindi.

 ambapo walisema elimu ambayo wameipata itawawezesha kutekeleza vema majukumu yao na hivyo kuweza kujiongezea pato na kukuza uchumi wao.



Akizungumza katika mkutano huo Baraza Seif ambaye ni Mkulima wa Mwani kutoka Kijiji cha Ndumbani aliwashukuru kwa kupatiwa elimu hiyo wakulima wa mwani na wavuvi ambayo itafungua ukurasa mpya katika shughuli zao

Alisema athari kubwa wanayokumbana nayo ni wavuvi wa nyavu aina ya kokoro waliopo kwenye maeneo ya Kata ya Moa na wavuvi wachache wanaotumia nyavu hizo kwenye kata ya Mayomboni na kutumia utupa ambao unaathiri Mwani wao.



“Hii ndio changamoto kubwa kwetu sisi wakulima hivyo Tunawaomba waache kwani kilimo cha Mwani kina faida kubwa kwenye maeneo sana ndani ya kata na nchi kilimo cha mwani ni zao endelevu mpaka kupelekwa nje “Alisema


Alisema kwamba jambo ambalo wanaliomba ni kuwepo kwa elimu endelevu kuhusu namna ya kuacha kuharibu zao za mwani kutokana na umuhimu wake katika kuwaingizia kipato cha mtu mmoja moja na jamii kwa ujumla.



“Tunaomba Shirika hili liweze kusimamia na kuturekebisha eneo hilo katika kata hizo mbili kutokana na baadhi yao kulima Mwani na wengine kuvua kwenye mashamba ya yao jambo ambalo linaleta uvunjifu wa amani wakati wa utekelezaji wa shughuli zao na kuathiri mkulima wa mwani kutokana na kwamba wanakwenda kuvua usiku.


Maeneo yanayolimwa mwani samaki wengi wanapwenda kwenda kuvua hapo hivyo wanaomba wavuvu waendele kupewa elimu kama wanahusika na mambo hayo waache maana kilimo cha mwani wanakitegemea kuendesha maisha yao na familia zao.



Naye kwa upande wake Mvuvi Salim Jumaa alisema kwamba kero yao watu wa mwani wanasema wavuvi wanaharibu mwani sio kweli kwa sababu hao watu wa mwani maeneo ambayo wavuvi wanayafanyia kazi wameyazuia na kuweka vigongo vyao ..

Hata hivyo Mkulima wa Mwani Kata ya Mayomboni Faida Bakari alisema wavuvi wanaposema wanawakosea maana wao ndio wana haribu kilimo cha Mwani kutokana wanapofika kwenye maeneo ya mashamba ya mwani wanang’oa vigongo na kuziachia kamba zinatembea.



“Sisi tunapoteza nguvu zetu unasema kuna kamba kumi unakuta zimeng’olewa na wanaweka utupa kuvua.hivyo tunaomba itungwe sheria ya kudhibiti vitendo vya namna hiyo katika maeneo yetu”Alisema


Kwa upande wake Mkazi wa Mayomboni Rehema Ally alisema athari kubwa ni wavuvi wa kukoro na wavuvi wanaotumia vyombo vikubwa na hivyo kuharibu mwani wao na mabadiliko ya tabia ya nchi yamewaathiri sana hivyo wanaiomba serikali wanapotoa malalamiko yao wapatiwe ufumbuzi hasa wale wanaovua uvuvi haramu.



Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahandakini Jasiri Nassoro Mbaraka alisema kwamba wanakuwa na makosa wakulima kama wanajua watu wanaoharibu mashamba yao ili pawe pazuri wanatakiwa wawaripoti kwenye vyombo vya kisheria.


“Lakini pia waweke hadharani kwanini mmetoka kule mnakuja kuvua huku kokoro ilipigwa marufuku isivue wanaowazungumza wavuvi wanavua kandondao ya kisiwa vya Kirui na kuna mashamba ya mwani na maeneo hayo yamewekewa zuio wasivue nadhani tunakuwa na makosa wakulima maeneo hayo yamewekewa zuio yasivuliwe na wanawaficha ili waweze kupata amani wakamatwa wafikishwe kwenye vyombo vya sheria”Alisema



Alisema kwani kuvua uvuvi haramu na kuharibu mashamba wakiendelea kuwaficha wavuvi wataharibu amani na haitapatikana mpaka wapelekewe kwenye vyombo vya sheria ili wachukuliwe hatua ili kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye mashamba ya mwani .



“Tukiendelea kuwaficha mgogoro huu hauwezi kupata ufumbuzi ili tutatue migogoro sheria zitumike wakulima wa mwani mnaona watu wanaharibu mwani mnaacha kuwasema sio sawa kwa maana palipowekewa zuio popote haparuhusiwi kufanya shughuli za uvuvi”Alisema



Akizungumza mmoja wa viongozi wa Shirika la Tawsei alisema lengo la mkutano huo ni kuana namna ya kupata ufumbuzi wa amani iliyopo nchini hivyo wanalishukuru Shirika la 4h Tanzania na wafadhili We World kushiriki pamoja kwenye mkutano huo.

Aidha pia walipendekeza kuwepo na ufumbuzi wa kutatua migogoro baina ya wakulima wa mwani na wavuvi wa samaki ili kudumisha na kuendeleza amani ya nchi y.  

Mradi huo unatekelezwa wilaya ya Mkinga katika kata mbili za Mayomboni na Manza ambao utakuwa chachu ya kutoa elimu itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na tija zaidi.



Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng