WASANII CHIPUKIZI WAMUOMBA RAIS SAMIA KUSHIRIKISHWA KUTANGAZA MAFANIKIO YA SERIKALI, CCM, UCHAGUZI MKUU

March 01, 2025



Mwenyekiti wa Mtandao wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni Tanzania (MMASUTA), Dkt. David Msuya (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Buguruni jijini Dar es Salaam, Machi 1, 2025.Kutoka kushoto ni Katibu wa mtandao huo, Jafari Makatu, Msimamizi wa Nidhamu wa mtandao huo, Kalethar Omari, Katibu Msaidizi wa Mtandao huo, Zainabu Jaha na Mwanakamati wa mtandao huo, Athuman Magenge.

...............................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WASANII Chipukizi kutoka Mtandao wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni Tanzania (MMASUTA) ambacho ndani yake kuna kikundi kinachoitwa Kazi Iendelee na Mama Samia, wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan awape nafasi ya kushirikishwa kunadi miradi ambayo imetekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 2025.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Dkt. David Msuya akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa utambulishaji wa kazi kadhaa za wasanii hao alisema wana muomba, Rais ili nao waweze sehemu ya timu ya kutangaza mafanikio mbalimbali yanayofanywa na Serikali.

 “Wasanii mnaowaona hapa leo wanavipaji vya aina tofauti tofauti kama vile uchezaji wa ngoma za asili, uigizaji, utunzi wa mashairi, ngonjera na uigizaji wa maigizo hivyo tukishirikishwa ipasavyo katika kazi mbalimbali za Serikali tutaweza kuzitangaza vyema kupitia vipaji vya wasanii hawa,” alisema Msuya.

Msuya alisema wasanii hao wanaimani na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla na wengineo.

Alisema wasanii hao chipukizi wamekaa na kutafakari na kuamua kumuomba Rais Samia awaweke katika timu ya itakayoshriki katika majukwaa yote ya kiserikali na kichama kwa pamoja kutangaza kazi ambazo zimetekelezwa na ili wananchi waweze kuzielewa kwa kina.

 “ Hapa kuna wasanii wenye vipaji vikubwa sana hivyo kama itampendeza Rais Samia ,kule anakokwenda kwa ajili ya ziara zake za kikazi kabla ya mkutano kuanza wasanii hawa waweze kutoa burudani, hivyo tunamuomba Rais na CCM kutuangalia kwa jicho la kipekee ili tuifanye kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa,” alisema Dkt. Msuya.

Katibu Mtendaji wa Mtandao huo, Jafari Makatu, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wasanii wa mtandao huo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wasanii wakiwa kwenye mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.
Taswira ya mkutano huo.
Makofi yakipigwa kwenye mkutano huo.
Kwaya ya mtandao huo ikitoa burudani.
Wasanii wa mtandao huo wakiigiza. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »