Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Juma Sweda anayemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka, leo Machi 15, 2025 amefanya mazungumzo mafupi na viongozi kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO).
Katika kikao hicho, Wizara ya Nishati iliongozwa na Mha. Ahmed Chinemba aliyemuwakilisha Kamishna wa Umeme Tanzania, Mha.Jones Olotu ambae ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini aliongoza timu ya Wakala wa Nishati Vijijini na TANESCO iliongozwa na Mha.Leo Mwakatobe ambae ni Meneja wa Mkoa Njombe.
Mazungumzo hayo yamelenga matayarisho ya ziara ya kupokea wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ambayo itafanya ziara ya siku 4 katika Mkoa wa Njombe kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.
EmoticonEmoticon