Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni miongoni mwa taasisi kutoka Tanzania zinazoshiriki maonesho makubwa ya Utalii duniani (ITB- Berlin) yanayoendelea kwenye jiji la Berlin nchini Ujerumani kwa lengo la kunadi vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zilizopo Nchini.
Zaidi ya makampuni 100 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar yanashiriki maonesho hayo ambayo yanahudhuriwa na makampuni ya utalii 5800 kutoka zaidi ya Nchi 170 Duniani.
Ujumbe kutoka Tanzania umeongozwa na Waziri wa Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mudrick Soragha, Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) ambapo NCAA imewakilishwa na Afisa Uhifadhi Mkuu- Utalii Bw. Peter Makutian
EmoticonEmoticon