WANAWAKE TUNAPOPATA FURSA TUSIMAME NA TUTENDE HAKI -MKURUGENZI UNUNUZI NISHATI

February 27, 2025

 


Mkurugenzi wa Ununuzi Wizara ya Nishati,  Bi. Marieta Kiago ametoa rai kwa Wanawake hususan vijana kuwa wanapopata nafasi za kufanyakazi kwenye maeneo na Taasisi mbalimbali kuhakikisha  

wanasimama imara na kuitenda haki kwa wananchi.


Bi. Kiaho ameyasema hayo alipokuwa akielezea nafasi ya Msichana katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo nchini yatafanyika mkoani Arusha.

"Ninachotaka kusema katika kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani wale tunaopata nafasi basi  tuzitendee haki hasa tunapotoa huduma kwa wananchi."  Amesema Bi. Kiago


Amesema miaka ya nyuma hakukuwa na haki kwa wanawake katika masuala mbalimbali tofauti na sasa ambapo haki za mwanamke zinazidi kutambuliwa na kuheshimiwa.


Akizungumzia  kuhusu usawa Bi. Kiago amesema  unatakiwa kuwepo katika jinsia zote kwa wanawake na wanaume ambapo ameipongeza Serikali kwa kuweka usawa katika utekelezaji wa majukumu kwenye jamii.


 Ameongeza kuwa kwa sasa wanawake wengi wameshika nafasi mbalimbali za uongozi akitolea mfano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »