UWANJA WA AFCON ARUSHA WAFIKIA ASILIMIA 25

February 03, 2025


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Arusha unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya mashindano ya Fainali za AFCON 2027 umefikia 25% za ujenzi wake.

Msigwa amesema hayo leo tarehe 3 Februari 2025 wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa uwanja huo unaojengwa katika kata ya Olmoti jijini Arusha.


Aidha, Msigwa amemtaka mkarandarasi anae Jenga uwanja huo wa kisasa wa Michezo wa Arusha kuongeza Kasi zaidi kwa kuzingatia viwango.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »