RC SENDIGA AMUAPISHA DC MBULU MICHAEL SEMINDU

January 29, 2025

 


Na Mary Margwe, Babati


Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Queen Cuthbert Sendiga amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mh. Michael John Semindu kuwa Mkuu wa wilaya ya Mbulu baada ya kuteuliwa na Mhe.Rais  tarehe 25 Januari,2025 kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Toka January 25, 2025


Hafla  ya uapisho huo imefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mjini ini Babati, huku viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya siasa na wa dini waliohudhiria hafla hiyo.



Akizungumza baada ya kukamilika kwa tukio la uapisho Sendiga alimpongeza Mkuu mpya wa Wilaya ya Mbulu kumshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza nguvu kazi ya watendaji katika Mkoa wa Manyara.


" Wakuu wa Wilaya Mimi kama kiongozi wenu, Nina vipaumbele nilivyojiwekea ili kufikia malengo ya pamoja ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa mapato ili Serikali iweze kuwahudumia Wananchi wake na kuleta maendeleo katika Taifa, kipaumbele Cha pili ni kusikiliza na kutatua za wananchi kuanzia Ngazi ya Mtaa mpaka katika Halmashauri zao Kwa wakati kipaumbele Cha tatu ni kusimamia ulinzi na usalama kwa kuweka mikakati ya kudhibiti Uhalifu, ioaumbele Cha nne ni kusimamia usafi wa mazingira ili kuweka Mkoa katika hali ya usafi pamoja na usimamizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo" amesema Queen Cuthbert Sendiga.



Aidha anafafanua kuwa anatambua kuwa kila mmoja qmejiwekea vipaumbele vyake kama Mkuu wa Wilaya husika, hivyo kama Mkoa pia una vipaumbele vyake ambavyo kila mmoja anatakiwa kuvielewa na hatimaye kuweza kuvirekeleza.



 “Naomba nendeni  mkatimize wajibu wenu ipasavyo na mkatekeleze  matarajio chanya  ya Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwani amewaamini na ndio maana amewapa nafasi hizo, hivyo ukiaminiwa, nawe unatakiwa ujiaminishe ili kuweza kutimiza adhima hii kikamilifu.” amesema  Sendiga.


Akizungumza mara baada ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mh. Michael John Semindu ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na watendaji wenzake pamoja na kuyapokea maagizo yote yaliyotolewa  na Mkuu wa Mkoa na kuyatekeleza majukumu yao yote kwa weledi mkubwa.


" Kwanza kabisa nimshukuru Mwenyezi Mungu aliyemuwezesha Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuniona na kuniteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, si kwamba mimi ni bora sna kuliko wengine  laa hasha, isipokua ni wakati wa Mungu umefikawa mimi kuonekana katika nafasi hii, hivyo nitatekeleza yote aliyoniagiza Mkuu wangu wa Mkoa " amesema Semindu.


Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mh.Semindu  kabla ya kuteuliwa na mh.Rais DKT. Samia kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, alikua ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »