KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA MASUALA YA UKIMWI YAKAGUA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA UKIMWI NJOMBE

January 09, 2025




NA.MWANDISHI WETU

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, imetembelea miradi mbalimbali  mkoani Njombe leo tarehe  09 Januari, 2025.

Kamati hiyo imetembelea kituo cha Afya cha Njombe Mjini kilichopo katika Halmashauri ya mji wa Njombe kwa lengo la kujionea huduma zinazotolewa katika kituo hicho ikiwemo huduma za upimaji UKIMWI, pamoja na kutembelea Shirika lisilo la kiserikali "COCODA"  linalohudumia watu wanaishi na virusi vya UKIMWI.

Kamati hiyo imeongozwa na  Mhe. Dr. Elibariki Kingu Mwenyekiti wa kamati na Mbunge wa Singida Magharibi, akiambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga


.

Aidha kamati imepokea taarifa ya mambukizi ya UKIMWI mkoani Njombe,  ambapo mkoa una watu 66,979 wanaishi na Virusi vya UKIMWI huku jitihada mbalimbali zikiendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na ugwaji wa kondom.

Hata hivyo kamati imetoa pongezi kwa Mkoa wa Njombe, kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Asasi zinazojihusisha na suala la kuhakikisha maambukizi ya VVU, yanapungua Mkoani Njombe.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga, ametoa shukrani kwa kamati ya kudumu ya Bunge, huku akiahidi Serikali kuendelea kushirikiana na wadau kwani bado kuna changamoto kubwa ya maambukizi ya VVU kwa vijana.




Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »