Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE), anaongoza vikao vya bodi ya taasisi hiyo jana nal eo Jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Vikao hivyo vilifunguliwa rasmi jana na Mhe. Reem Al Hashimy, Waziri wa Nchi wa UAE anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa. Umoja waFalme za Kiarabu umekuwa mshirika muhimu wa GPE kwa miaka kadhaa.

Vikao hivyo vinawakutanisha wajumbe wa bodi wakilisha wa nchi mbalimbali, mashirika yakimataifa, na vyama vya kiraia kutoka pande zote za dunia.
Miongoni mwa wahudhuriaji mashuhuri alikuwa Mhe. Prof. Nasser Al Aqeeli, Naibu Waziri wa Elimu wa Saudi Arabia, aliyeelezea dhamira ya Ufalme wa Saudi Arabia kuendelea kushirikiana na GPE katika kutatua changamoto za elimu msingi (chekechea, elimu ya msingi, na sekondari) katika nchi zinazoendelea.

GPE ni mpango wa kimataifa unaolenga kuboresha elimu katika nchi zinazoendelea, hasa kwa watoto waliotengwa au wanaokosafursa.

Ukiwa imeanzishwa mwaka 2002, GPE inasaidia elimu ya awali, msingi, na sekondari kwa kuzingatia usawa, ujumuishi, na ubora wa masomo.
Shirika hili pia huhamasisha rasilimali, kushirikiana na serikali, mashirika ya kiraia, na taasisi za kimataifa, na hutoa ruzuku zinazolenga matokeo.
Kwa kuimarisha mifumo ya elimu, GPE linaendana na Lengo la Maendeleo Endelevu 4, kuhakikisha elimu jumuishi na bora.

Tayari limebadilisha maisha ya mamilioni ya watoto katika nchi zaidiya 90 kwa kuwapa fursa ya elimu bora na maendeleo endelevu.

EmoticonEmoticon