DC SUMAYE AONGOZA WANANCHI ZOEZI LA KUJIANDIKISHA

October 12, 2024

 Na Ashrack Miraji Lushoto Tanga


MKUU wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Zephania Sumaye amesema zoezi la undikishaji wananchi kwenye daftari la mkazi linaendelea vizuri, wananchi wamehamasika vituo vingi wameshajiandikisha na bado wanaendelea kujiandikisha.

DC Sumaye amezungumza hayo Oktoba 11 mwaka huu 2024 mara baada ya kujiandikisha katika daftari la mkazi kwenye Kituo Cha Chake Chake ambacho ni miongoni mwa kituo cha uandikishaji wananchi kwenye daftari la makazi

Aidha amesisitiza wananchi wakazi wa Lushoto kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vilivyopo kwenye maeneo yao kujiandikisha ili wawe na uhalali wa kupiga kura Novemba 27 mwaka huu 2024.

“Tayari kama Mkuu wa Wilaya nimejiandikisha, lakini pia nimepata nafasi ya kukagua baadhi ya vituo kuona hili zoezi linaendaje, nimefarijika sana zoezi linaendelea vizuri Wananchi wamehamasika vituo vingi wameshajiandikisha na bado wanaendelea kujiandikisha”. Alisema DC Sumaye

Zoezi la Uandikishaji wananchi kwenye daftari la mkazi limeanza rasmi leo Oktoba 11 na linaendelea hadi kufikia Oktoba 20 mwaka huu 2024.

Kauli mbiu “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi”



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »