TBS YAENDELEA KUTOA ELIMU YA VIWANGO NANENANE LINDI

August 04, 2024

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewashauri wajasiriamali kuzingatia matakwa ya kisheria katika masuala ya afya,usalama na mazingira kwenye usindikizaji wa bidhaa mbalimbali kwa lengo la kuzalisha bidhaa bora na salama.

Akizungumza Agosti 03, 2024 katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi Meneja wa TBS, Kanda ya Kusini Mhandisi Said Mkwawa amesema TBS kama chombo. chenye dhamana ya kusimamia viwango vya kitaifa wameona ni vyema kutoa elimu kwa umma ili kuhakikisha zinazalishwa biidhaa bora ili kulinda afya ya mlaji.

Aidha Mhandisi Mkwawa ametoa rai kwa wajasiriamali kujitahidi kutengeeneza bidhaa ambazo zinakidhi matakwa ya viwango. vya. ubora ili kulinda afya ya watumiaji wa bidhaa. hizo na kuepuka kuzalisha bidhaa zilizo chini ya viwango kwani zinahatarisha afya,uchumi na usalama.

"Kamwe Shirika la Viwango haturuhusu iwe kutengeneza au kuingiza nchini bidhaa zote zenye viwango hafifu kwani zitaleta athari kiuchumi,kiafya na kiusalama kwa ujumla" amesema Mhandisi Mkwawa

Pamoja na hayo ameeleza kuwaTBS imekuwa na utaratibu wa kufanya kaguzi mara kwa mara kwenye maeneo ya uzalishaji ili kubaini makubaliano yao na mzalishaji kama bado yanazingatiwa. kwa lengo la kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa bidhaa hizo.

TBS imekuwa ikuonesha nia yake ya dhati ya kuwainua wajasiriamali ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora sambamba na kuwapatia alama ya ubora ambayo itawasaidia kukuza wigo wa soko lao nchini na kimataifa ambapo imekuwa ikiwahimiza kukagua bidhaa zao ili kujiridhisha kuhusu ubora wake ambapo itawapatia mwanya wa kupata ushauri jinsi ya kuboresha kunapokuwa na uhafifu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »