TPA IPO KATIKA HATUA NZURI UJENZI WA KITUO JUMUISHI CHA KUPOKEA MAFUTA

January 14, 2024






Na Sophia Kingimali

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema ipo kwenye hatua nzuri ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo jumuishi cha kupokea mafuta eneo la Kigamboni na Kurasini,ili kutatua changamoto ya meli za mafuta zinazoingia katika bandari hiyo kukaa kusubiri muda mrefu kwa ajli ya kushusha shehena ya mafuta.

Hayo ameyasema leo Januari 14,2024 jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho wakati wa ziara yake na waandishi wa habari katika bandari hiyo ili kujionea maboresho mbalimbali yanayofanyika katika bandari hiyo ikiwemo upanuzi wa lango la kuingilia meli.

Amesema ujenzi wa kituo hicho cha kuhifadhia mafuta kitapunguza gharama na kurahisisha utendaji kazi ambapo watu wote watakua wanaenda kuchukulia mafuta hapo na si kama ilivyo sasa ambapo mafuta yanapelekwa katika kampuni binafsi.
- Advertisement -

Ameongeza kuwa uongezaji wa kina kwenye bandari hiyo kutoka mita tisa hadi kufikia mita 14 umeendelea kuchagiza uingiaji wa meli kubwa zenye urefu wa mita hadi 200 tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Pamoja mambo mengine Mrisho ameweka bayana kuwa bandari hiyo imedhamiria kuvuka malengo yaliyowekwa na serikali katika mwaka wa fedha 2023/24 ya utoaji wa huduma ya mizigo kutoka tani milioni 22 hadi milioni 24 kutokana na maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika.

Akizungumzia eneo la kuhudumia magari amesema eneo hilo la mita 320 linahudumia magari 6000 kwa mwezi huku kwa mwaka yakiwa magari 250,000 mpka 300,000.

“Eneo hili la magari linamifumo ya ulinzi na usalama na hii imesaidia kuondoa changamoto ya wizi wa vifaa vya magari iliyokuwepo awali”amesema Mrisho.

Aidha Mrisho amesema pamoja na kuwa na ufanisi mkubwa unaofanyika kwenye bandari hiyo lakini pia kunachangamoto kwenye upakuaji wa baadhi ya mizigo hasa kwenye kipindi cha mvua.

Amesema kuna baadhi ya mizigo kama mbolea,ngano zinaathiliwa na mvua hivyo katika kipindi hiko huduma zinakuwa zinathitishwa ili kuepuka uharibifu.

“Hizi product hazihitaji maji ukilazimisha unakua unaharibu meli kama hii ya baric yenye tani 49,000 mpka 50,000 kama utaweka tageti ya huihudumia kwa siku saba au tano siku lazima zitaongezeka hivyo mvua zinazonyeesha zinaathiri utendaji kazi”amesema.

Aidha ameongeza kuwa ongezeko la meli bandarini ni ufanisi mkubwa wa bandari hiyo hivyo ongezeko hilo linasaidia kuongeza mapato kwa nchi na kuinua uchumi.

Amesema kwa kuanzia ijumaa januari 12,2024 mpka jumatatu januari 15 wanatarajia kupokea meli mpya 16 zitakazoingia nchini ili kupata huduma ambapo amesema wajibu wa bandari ni kuongeza spidi ya kuzihudumia.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »