PSPTB YAFIKA CHUO KIKUU MZUMBE KUTOA ELIMU

June 05, 2023

 Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo Wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo Kikuu Mzumbe hii ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu kwa umma hasa kwenye vyuo vinavyotoa masomo ya Ununuzi na Ugavi.


Akizungumza na Michuzi Blog, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema Bodi hiyo imeendelea kuwapa mafunzo Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wanaochukua kozi hiyo ya Ununuzi na Ugavi kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi, Usajili kwa njia ya mtandao, mtaala mpya, pamoja na maadili na miiko ya taaluma hiyo.

Mbanyi amesema mtaala huu mpya utaanza kutumika kwenye mitihani ijayo ya mwezi wa 11 ambapo wahitimu wote watautumia hivyo wanapita vyuoni kutoa elimu ili wanapomaliza vyuo waweze kuendana na mtaala huo mpya.

Naye, Mkuu wa Idara ya Ununuzi na Usimamizi wa Vifaa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Paul M. Nsimbila ametoa shukrani kwa wafanyakazi wa PSPTB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi kwa kuweza kufika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na Wanachuo pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuhusu namna Bodi hiyo inavyowasimamia Wataalam wa Ununuzi na Ugavi wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo hicho.
Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Mjini Morogoro.
Afisa Elimu Mkuu- Mitaala (PSPTB), Jeremiah J. Haule akitoa mada kuhusu namna ya kuongeza dhamani pamoja namna walivyobadili mtaala kwenye taaluma ya Ununuzi na Ugavi kwa wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Mjini Morogoro ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
Afisa TEHAMA kutoka PSPTB Boniface Mushi akitoa mada kuhusu namna ya mwanafunzi anavyoweza kujisajili pamoja na kufanya mitihani ya Bodi wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Mjini Morogoro ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo Kikuu Mzumbe wakiuliza maswali mara baada ya wataalam kutoka PSPTB kuwasilisha mada mbalimbali chuoni hapo.
Mkuu wa Idara ya Ununuzi na Usimamizi wa Vifaa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Paul M. Nsimbila akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wa PSPTB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi waliofika chuoni hapo kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi.
Baadhi ya wanafunzi wa Shahada na Shahada ya Uzamili wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo Kikuu Mzumbe wakifuatilia mada kutoka kwa wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) waliofika chuoni hapo kwa akili ya kutoa elimu zinayohusu Bodi hiyo.
Picha ya Pamoja

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »