Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala akisisitiza jambo kwa wadau wa sekta ya Uchukuzi kwa njia ya maji na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza na Mikoa ya Jirani(hawapo pichani) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Tarehe 25 Juni,2023
Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi Bi Stella Katondo akisisitiza jambo kwa Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala na Baadhi ya Mabaharia, Wafanyakazi wa wizara, Taasisi na Wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Jiji la mwanza na Mikoa ya jirani (hawapo pichani) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Tarehe 25 Juni,2023
Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi Bi Stella Katondo akimuongoza Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala kukagua mabanda ya maonesho ya wadau wa usafiri kwa njia ya maji wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Tarehe 25 Juni,2023
Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala akigawa vyeti vya pongezi kwa Mabaharia waliofanya Vitendo vya kijasiri vya uokozi kwa nyakati mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Tarehe 25 Juni,2023
Baadhi ya Mabaharia, Wafanyakazi wa wizara, Taasisi na Wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Jiji la mwanza na Mikoa ya jirani wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala ( katikati kwa waliokaa) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Tarehe 25 Juni,2023

Baadhi ya Mabaharia, Wafanyakazi wa wizara, Taasisi na Wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Jiji la mwanza na mikoa ya jirani wakifuatilia mada kutoka kwa Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Tarehe 25 Juni,2023
Kwaya ya Watumishi wa Jiji la Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi Bi Stella Katondo walipotembelea banda la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Tarehe 25 Juni,2023
Baadhi ya Mabaharia, Wafanyakazi wa wizara, Taasisi na Wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Jiji la mwanza na Mikoa ya jirani wakiwa kwenye picha ya pamoja na Medali zao mara baada ya kumaliza kushiriki mbio za KM 7 za Seafarers Marathon zilizoanzia kwenye Mwalo wa Kirumba na kumalizikia kwenye viwanja vya Furahisha ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Tarehe 25 Juni,2023

Na Mwandishi wetu Mwanza
Serikali imewataka Mabaharia kote Nchini kuzidi kujiendeleza kielimu na kuchapa kazi kwa bidii ili waaminike kwenye ajira hususan za kimataifa ili waweze kupata fursa zaidi za kufanya shughuri za ubaharia nje ya Nchi kwa manufaa yao na Nchi kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo na Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Masala wakati wa akihitimisha maonesho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza kuanzia Tarehe 22 Juni, 2023 na kufikia tamati Tarehe 25 Juni,2023.
Mhe.Masala amesema Mabaharia huendesha na kuwezesha uchumi wa nchi zao na Dunia kukua, kwa kulitambua hilo Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Awamu ya Nane ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Mhe. Dkt Hussein Ally Mwinyi kwa kushirikiana na vyama vya Mabaharia, wamiliki wa vyombo vya usafiri majini na taasisi mbalimbali za kimataifa zimefanya kila liwezekanalo kuhakikisha kazi za Ubaharia na taaluma yake zinatambuliwa nchini na nje ya nchi sasa kuliko wakati mwingine wowote ule.
“Serikali imehakikisha Mabaharia wanapewa heshima inayostahili kama zilivyo taaluma nyingine sasa ni wakati wenu sasa Mabaharia kote Nchini kutumia fursa hii kujiendeleza zaidi kitaaluma ili mzidi kuaminika kwenye ajira za kimataifa” amesisitiza Masala
Mhe. Masala amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawajali sana Mabaharia kwani katika mkoa wa Mwanza imekarabati Meli za MV Victoria , MV Butiama,Mv Umoja na kujenga meli mpya ya MV Mwanza ambazo zitasaidia kuongeza upatikanaji wa ajira kwa Mabaharia
Akimkaribisha Mgeni rasmi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi Bi.Stella Katondo amesema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiunga na Shirika la Bahari Duniani(IMO) lenye majukumu ya kukuza na kusimamia utendaji wa Sekta ya Usafiri majini, kusimamia ulinzi, usalama na uhifadhi wa mazingira ya maji tangu mwaka 1974 ambapo walikubaliana Kusherehekea Siku ya Mabaharia Duniani kila mwaka ifikapo tarehe 25 Juni,2023
Bi. Stella amesema Maadhimisho haya ya siku ya Mabaharia Duniani yanayoambatana na kauli mbiu
“Miaka 50 ya MARPOL uwajibikaji wetu unaendelea” yaliyofanyika Kitaifa Jijini Mwanza kuanzia tarehe 22 Juni,2023 na kufikia tamati tarehe 25 Juni,2023 yalikutanisha Taasisi, Wizara na wadau wote wa Sekta ya Uchukuzi kwa njia ya Maji Nchini kwa lengo la kutambua umuhimu wa kazi ya Mabaharia na kuwaenzi mabaharia ambao ni kiungo muhimu sana kwa uchukuzi kwa njia ya maji na kukuza uchumi wa Taifa na Dunia
Maonesho ya siku ya Mabaharia Duniani yaliyoanza tarehe 22 mpaka 25 Juni, 2023 na kufanyika kitaifa Jijini Mwanza yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta Uchukuzi kwa Tanzania Bara kupitia Shirika la uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) na Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Zanzibar(ZMA), Pamoja na wadau mbalimbali wa Uchukuzi kwa njia ya maji Nchini.

EmoticonEmoticon