Na Oscar Assenga,TANGA
JUMLA ya Mikataba 8 ya miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 10 itakayotekelezwa katika wilaya tano za mkoa Tanga imesainiwa mwishoni mwa wiki na Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa huo pamoja na mkataba mmoja wa mhandisi mshauri .
Miradi hiyo ya maji itakwenda kuwa mkombozi na kwa wananchi kwenye vijiji 20 wapatao 39, 226 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2023 sawa na asilimia 1.5 ya wakazi wote wa mkoa huo.
Akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upenndo Lugongo alisema miradi hiyo ambayo ni mipya yenye jumla ya vituo 92 vya kuchotea maji na matangi 9 yenye ujazo wa jumla ya mita za ujazo 1,830.
Mhandisi Upendo alisema pamoja na mtandao wa mabomba kilometa 162.2 inatarajiwa kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 1.5 kwa wananchi wanaoishi vijijini.
Alisema kwamba lengo la kusainiwa kwa mikataba hiyo ni kuingia makubaliano ya pamoja na wakandarasi pamoja na mhandisi mshauri ambayo yataleta ufanisi na tija ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kufuata kanuni , taratibu na sheria mbalimbali zitakazofuatwa kwa nia ya kukamilisha utekelezaji huo.
Alisema licha ya miradi hiyo mipya kusainiwa ipo mingine minne inatekelezwa ikiwa ni mkakati wao wa kuhakikisha wanaondosha changamoto ya ukosefu wa maji vijijini katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga ambapo jumla ya wananchi 2, 310000 wanatarajiwa kunufaika mara baada itakapokamilika.
Hata hivyo alisema katika miradi hiyo inayoendelea itakapokamilika itaweza kusaidia kuwahudumia wananchi wapatao 2, 31000 sawasawa na asilimia 9 ya wakazi wa mkoa wa Tanga ukilinganisha na ile ya mwaka 2022, tunaenda kusaini mikataba 9 ambayo ni ndani ya ujenzi lakini pia kuna mkataba mmoja wa mhandisi mshauri na katika mikataba hii nane tunaweka kwanza mabomba yenye jumla kilometa 1, 68, 000 ambayo ina thamani yabshilingi bilion 10 na inaenda kujenga vituo 110 ambavyo tutakuwa tunahudumia wakazi 31, 0000 "
"Lengo kuu la serikali ni kuhakikisha tunamtua mama ndoo kichwani na kuona kwamba huduma ya maji tunaenda kuitoa na kupunguza muda wa utafutaji maji kwa wananchi ili waweze kushiriki kwenye kazi nyingine za kiuchumi , serikali inaelekeza kuwa ifikapo 2025 tuwe tumefikia asilimia 85 ya upatikanaji wa maji vijijini" alisema Lugongo
Alisema kwamba wakala huo umeingia makubaliano na makambuni mbalimbali ambayo ni kampuni ya Nipo Africa engineering Co.ltd atakayetekeleza miradi katika wilaya ya Kilindi , Lukedan Company Limited wilaya ya Handeni, Wraptec engineering ltd Handeni, Planet water Geographycs ltd (Mkinga), Wraptec engineering ltd (Korogwe), Buzubona and Sons Company na Hinry Company (Lushoto) pamoja na kampuni ya Env Consultant
Akizungumza wakati wa halfa hiyo Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewataka wakandarasi wote watakaotekeleza miradi hiyo ambao wengi wao ni wazawa kuwa wazalendo na kukamilisha kazi kwa wakati ili iweze kuleta tija kwa wananchi ikiwemo kuwataka kuwatumia wananchi wa maeneo husika wakati wa utekelezaji wa mradi huo
"Fedha hizi ni nyingi sana ambazo ni kodi za watanzania hivyo zinatakiwa zionyeshe matokeo makubwa yenye tija kwa miundombinu ya maji inayotumiwa na wananachi ili kukidhi malengo ya serikali, nimeelezwa kuwa sehemu kubwa ya wakandarasi wanaotekeleza miradi hii ni wazawa hivyo nawataka kuwa wazalendo kwa kufanya kazi weledi na ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa mikataba hii nasisitiza wakandarasi kuwatumia wananchi wa maeneo inayotekelezwa miradi hii katika kazi za vibarua ambazo hazihitaji utaalam mkubwa" alisema Mgumba.
Rc Mgumba amewataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kuyatunza mazingira sambamba na kujiepusha na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji ambapo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikichangia kukosekana kwa huduma hiyo na hatimaye kusababisha athari mbalimbali ikiwemo changamoto ya maji ya kutosha pamoja na ukame katika vyanzo vikubwa vinavyotegemewa na mamlaka husika.
"Kuna changamoto ya upatikanaji wa maji safi na yamekuwa haba ni kwa sababu ya ukame ambao umesababishwa na uharibifu wa mazingira na ukame ikiwemo shughuli za kibinadamu na kuvamia vyanzo vya maji nitoe wito kwa wananchi tutunze mazingira ili nayo yatutunze ili kuondokana na uhaba huu wa maji ili mito yetu iwe na maji muda wote"
"Tuna tatizo kubwa la uhaba wa maji katika mkoa wetu wa Tanga na moja wapo ya sababu ni kutokana na umeme mdogo tuliokuwa nao unakatika mara kwa mara na hautabiriki kwahiyo tuna uhaba zaid ya Mega wat 20 zinazohitajika mahitaji yetu yalikuwa zaid ya megawa 136 lakini sasa zimeshuka hadi 80" alibainisha Mgumba
EmoticonEmoticon