
Mheshimiwa Hussein Bashe Waziri waKilimo akizungumza wakati akifungua semina ya siku mbili iliyowahusisha wadau wa Sekta ya Umwagiliaji mjini Morogoro

Mheshimiwa Hussein Bashe Waziri waKilimo akizungumza wakati akifungua semina ya siku mbili iliyowahusisha wadau wa Sekta ya Umwagiliaji mjini Morogoro

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,Bw, Raymond Mndolwa akizungumza wakati wa semina hiyo

NA MWANDISHI WETU,MOROGORO
Waziri wa
Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe, amesema kwa Mwaka wafedha ujao Wizara
yake itatumia Shilingi Bilioni 420 katika ujenzi wa Miundo mbinu ya
Skimu za umwagiliaji ikiwemo Hekta elfu kumi kwa ajili ya uzalishaji wa
Mbegu ambapo wadau wa sekta binafsi watapewa kipaumbele kwa ajili ya
kuzalisha Mbegu, ujenzi wa mabwawa 14 yatakayokuwa na miundombinu ya
umwagiliaji kwa matumizi ya kilimo na mifugo.
Eneo lingine la kipaumbele kwa Waziri Bashe ni pamoja na kuwasaidia Wakulima Wadogowadogo kupataTeknolojia bora za kilimo cha umwagiliaji kwa bei nafuu ili waweze kupata tija na kuchangia ongezeko la mavuno katika sekta ya umwagiliaji, zoezi hilo litawahusu pia Vijana wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw,Raymond Mndolwa amewataka watumishi wote wa tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufanya kazi kwa bidi na ubunifu ili kutimiza matarajio yaliyowekwa na serikali, akiamini taasisi yake inauwezo wakutekeleza majukumu yaliyopangwa na serikali kwa wakati, ufanisi na ubora unaotakiwa katika kuhudumia wananchi.
“ Nitamsapoti kila mtumishi aweze kutimi za wajibu wake, tumejipanga na lililopo mbele yetu tunaweza kulitekeleza”
Semina hiyo ya siku mbili imewashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi, Wakulima wadogo, Wataalam waBenki, Vyama vya Ushirika, Wahandisi na Maafisa kilimo wa Wilaya ikiangazia namna ya kuboresha maeneo matatu muhimu katika kilimo cha umwagiliaji ,uzalishaji, huduma za u mwagiliaji na njia bora yakukusanya Ada naTozozaUmwagiliaji.
EmoticonEmoticon