Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema
Tanzania inakwenda kushirikiana na klabu ya Soka ya Southampton
kuwandaa makocha wa soka ili wawe kwenye kiwango cha kimataifa.
Mhe.
Mchengerwa amesema haya leo juni 17, 2022 ofisini kwake akiambatana na
Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dk. Hassan Abbasi wakati alipokutana na
ujumbe wa Klabu hiyo ulioongozwa na Afisa Biashara Mkuu wa Klabu hiyo
David Thomas.
Amesema
dhamira ya Serikali ni kuona kuwa michezo mbalimbali inasimamiwa
kisayansi ili kuleta tija ikiwa ni pamoja na kuwa na makocha ambao
watasaidia kufundisha timu za micherzo ili kufuka kwenye kiwango cha
kimataifa.
Katika
kikao hicho wamekubalina kuwa Timu ya soka ya ya Wanawake chini ya
Miaka 17 (Serengeti Girls) itakwenda kupatiwa mafunzo maalum kwenye
Klabu hiyo ikiwa ni maandalizi ya kwenda kwenye mashindano ya kombe la
dunia nchini India.
Katika
tukio hilo ujumbe wa timu hiyo ulimzawadia jezi Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kuthamini mchango
wake mkubwa anaoutoa kuendeleza michezo nchini.
EmoticonEmoticon