WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Innocent Bashungwa
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Innocent Bashungwa amesikia kilio
cha Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina aliyehoji sababu ya Serikali
kutozifungua Zahanati 10 zilizojengwa na kukamilika kwa miaka mingi sasa
huku wananchi wa vijiji hivyo wakilazimika kutembea umbali mrefu
kutafuta huduma.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Afya bungeni
Dodoma Mei,2022, Mpina alisema upungufu wa watumishi wa kada ya Afya
ngazi ya Zahanati ni tatizo ambalo halijapata suluhu kwa muda mrefu na
wananchi wakiendelea kukosa huduma hitajika katika vijiji vingi vya
Jimbo la Kisesa.
Mpina alisema Serikali ilipaswa kuweka
utaratibu mzuri wa ajira na kutumia njia mbadala ya kuingia 4 mkataba na
vijana waliohitimu mafunzo mbalimbali ya Afya ambao hawaja ajiriwa ili
kusaidia utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Mheshimiwa Spika,
Kwenye Jimbo langu la Kisesa nina Zahanati 10 zilizokamilika muda mrefu
lakini huduma hazitolewi, Mfano Zahanati ya Kijiji cha Semu, Mwandu
Kisesa, Makomangwa, Mwageni, Mwagayi, Isangijo, Ikigijo, Mwakisandu,
Malwilo na Tindabuligi, lakini pia tuna maboma ya muda mrefu 10 ya
Kijiji cha Inonelwa, Mwamhongo, Nzanza, Matale, Masanga, Mwakipugila,
Ntobo, Ng’hanga, Mwakasumbi na Lubiga” alisema Mpina.
Hata hivyo
kwa mujibu wa orodha ya majina ya watumishi wapya wa sekta ya Afya
iliyotangazwa na Waziri Bashungwa Juni 26, 2022 kwa Jimbo la Kisesa
zitafunguliwa Zanahati 6 kati ya 10 zilizokamilika ujenzi wake.
Waziri
Bashungwa amezitaja Zahanati hizo mpya zilitakazofunguliwa rasmi kwa
Jimbo la Kisesa na idadi ya watumishi wapya kwenye mabano kuwa ni
Zahanati ya Kijiji cha Isangijo Kata ya Lubiga (3), Zahanati ya Kijiji
cha Makomangwa Kata ya Mwandoya (3), Zahanati ya Kijiji cha Mwagayi Kata
ya Itinje (3).
Pia Waziri Bashungwa amezitaja zahanati nyingine
zitakazofunguliwa Jimbo la Kisesa kuwa ni Zahanati ya Mwageni Kata ya
Isengwa (3), Zahanati ya Kijiji cha Mwasungura Mwageni B (2), Zahanati
ya Kijiji cha Malwilo Mnadani Kata ya Tindabuligi (3), Zahanati ya
Mwandu Kisesa Kata ya Kisesa (3).
Waziri Bashungwa amewataja
watumishi hao na majina ya vituo vyao kwenye mabano kuwa kuwa ni Teodora
Kalistus Chodota Muuguzi Daraja la II, Ayubu Gladwell Mwaibosi Muuguzi
Daraja la II na Ramadhani Shabani Mrutu, Tabibu Daraja la II (Co)
(Zahanati ya Isangijo).
Wengine ni Joseph Rashid Ghake, Muuguzi
Daraja la II, Edomu Anania Mwakingwe, Muuguzi Daraja La II, Frank John
Mandala Tabibu Daraja la II (Zahanati ya Makomangwa).
Bashungwa
amewataja wengine kuwa ni Nuru Daud Mwala , Muuguzi Daraja la II na
Ernest Joseph Kachwele, Muuguzi Daraja la II (Zahanati ya Malwilo).
Wengine ni Samwel Gelewa Simon, Muuguzi Daraja la II, Maryam Baraka
Omar Female, Tabibu Daraja la II (CO) na Yohana Magori Magori, Muuguzi
Daraja la II (Zahanati ya Mwagayi).
Wengine ni Azizi Poul
Mgoboleni, Tabibu Daraja La II (Co), Johnson Joseph Kayombo, Muuguzi
Daraja la II na Damian Emanuel Lyimo, Muuguzi Daraja la II (Zahanati ya
Mwageni). Bertha Juvenary Nyamwiula, Muuguzi Daraja la II na Nkeshimana
Jumanne Kasonga, Muuguzi Daraja la II (Zahanati ya Mwageni B-
Mwasungura).
Wengine ni Kissile Nelson Mwakabago, Muuguzi Daraja
la II, Eufransia Zacharia Mjuanga, Muuguzi Daraja la II na Ezekiel
Christopher Mantyotyo, Tabibu Daraja la II (Co) (Zahanati ya Mwalilo
Mnadani). Watumishi wengine ni Thereza Revocatus Lweyemaho, Muuguzi
Daraja la II, Kasilda Gervas Nkembo, Tabibu Daraja la II (CO) (Zahanati
ya Mwandu Kisesa).
TANGA RAHA BLOG
habari
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA MBUNGE MPINA UKOSEFU WA HUDUMA KWENYE ZAHANATI JIMBO LA KISESA
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon