"Hapa Tanzania wanazungumza Kiswahili na baadhi ya lugha za nje na hili linafungua milango ya ajira ndani ya Tanzania na nje ya nchi kwa wanaozungumza Kifaransa na ndiyo maana tunatangaza lugha hii ili watu waitumie."
"Tanzania inapakana na nchi nchi nyingi ambazo zinazungumza Kifaransa hivyo ni muhimu Kifaransa kufundishwa katika shule na vyuo vikuu kwa manufaa ya Watanzania ambao wanatamani kupata nafasi katika nchi zinazozungumza Kifaransa," alisema Clavier.
Aidha, Clavier alizungumzia Wiki ya Francophonioe na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika maonesho mbalimbali yaliyoangaliwa na OIF ambayo yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa, Allience Française, Century Cinemax ya Oysterbay na Jakaya Kikwete Omnisport Park iliyopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
--
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »