MASHINDANO ya ndani ya mchezo wa Pool Table mkoa wa Tanga yanatarajiwa
kuanza kutimumia Machi 3 mwaka huu kwenye ukumbi wa Kichuya Pub
itakayohusisha timu zinazomaliza Ligi ya mkoa msimu uliopita na
kufanikiwa kuingia sita bora.
Ukumbi huo upo wilayani Korogwe ambapo msimu huu wamepaanga kuchezesha timu sita badala ya kumi kama ilivyokuwa miaka iliyopita kutokana na makubaliana yao na mfadhili ambaye atadhamini mashindano hayo.
Akizungumza na Tanga Raha Blog,Katibu wa Chama cha Mchezo wa Pool Table mkoa wa Tanga(TARPA) Shabani Kibelo alisema msimu huu wamepanga mashindano hayo kuchezwa kwa siku tatu.
Alisema katika mashindano hayo ambayo yamefadhiliwa na mdau mmoja mkoani Tanga yatafanyika kwa ufanisi mkubwa huku kila timu shiriki ikigharamiwa fedha za usafiri wa kwenda na kurudi.
Kibelo alisema katika mashindano hayo mshindi wa kwanza kwa timu ataapata sh.500,000 mshindi wa pili sh.300,000 mshindi wa tatu akipata sh.200,000.
Alisema pia kwa washindi mmoja mmoja ambapo kwa upande wa wanaume mshindi wa kwanza atapata sh.300,000 mshindi wa pili sh.200,000 huku mshindi wa tatu akipata sh.100,000.
Hata hivyo aliongeza kwa upande wa wanawake mshindi mmoja mmoja wa kwanza sh.200,000 mshindi wa pili atapata sh.100,000 na mshindi wa tatu atapata sh.50,000.