Na John Nditi, Kilombero.
HALMASHAURI
ya wilaya ya Kilombero , mkoani Morogoro wamewakatia kadi za Mfuko
wa Afya ya Jamii (CHF ) iliyoboreshwa wazee wasiojiweza zaidi ya 7,800
waliopo katika kata 26 ili kuwawezesha kupata huduma bora za
matibabu katika vituo vya Afya, Zahanati na hospitali na wategemezi
wao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri hiyo , Dennis Londo alisema hayo mbele ya
Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, kabla ya zoezi la
ugawaji kadi za CHF Iliyoboreshwa kwa baadhi ya wazee wapatao 2,100
kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
Londo
alisema kuwa , hadi sasa kiasi cha Sh milioni 13.3 zimetumika kwa
ajili ya mpango wa kuwakatia wazee wasiojiweza bima ya afya ya CHF
Iliyoboreshwa.
Hata
hivyo alisema , halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha wazee
wanapatiwa bima ya Afya CHF iliyoboreshwa na lengo ni kuwafikia wazee
wasiojiweza zaidi ya 15,000 katika kata zote 26.
“
Halmashauri ya wilaya hii imejipanga vyema na inatekeleza ilani ya
uchaguzi ya CCM na miongoni mwa mam ohayo ni kundi la wazee wasiojiweza
wamenufaka na huduma ya bima ya afya” alisema Londo.
Naye
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo , David Ligazio aliwataka watendaji wa
vituo vya afya, zahanati na hospitali ambaki madirisha ya wazee
hayajaanzishwa waanzishe mara moja ili wazee hao wapate unafuu wa
huduma kulingana na lengo lililokusudiwa .
Kwa
pande wake mkuu wa wilaya ya Kilombero , James Ihunyo alisema ,
halmashauri hiyo inaendelea kufanya vizuri kutokana na sehemu ya fedha
zinazopatikana za makusanyo ya ndani kuelekezwa kuboresha huduma za
kijamii ikiwemo kuwakatia bima ya afya wazee wasiojiweza sambamba na
kwa halmashauri ya mji Ifakara.
Awali
akisoma taarifa ya ugawaji wa kazi hizo , Ofisa Elimu Kata
Kalengakelu, Zainab Said alisema, wazee wasiojiweza walionufaika na
mpango huo ni wa kutoka kwenye vijiji 23 vya kata ya Chisano,
Kalengakelu, Mlimba, Kamwene, Utengule , Masagati na Uchindile .
Akizungumza
katika halfa hiyo katibu tawala wa mkoa huo, Tandari alizitaka
halmashauri nyingine ndani ya mkoa huo kuiga mfano wa halmashauri ya
wilaya ya Kilombero ili kuhakikisha wazee wote wanakuwa bima ya afya.
Nao
baadhi ya wanufaika na mpango huowa CHF iliyoboreshwa ,Nelasi Nyingi
na Petro Karubandika kwa nyakati tofauti waliipongeza Serikali na
uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero kwa kuwawezesha kuingizwa
kunufaika na huduma za afya hasa ikizingatiwa wao wanahauwezo wa
kifedha na wategemezi wao.
Katibu
Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kushoto)
akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
Iliyoboreshwa mzee Petro Karubandika mkazi wa kata ya Mlimba ,
halmashauri ya wilaya ya Kilombero wakati wa zoezi la ugawaji kadi
hizo kwa wapatao 2,100 kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya
Mlimba na ( kushoto) ni mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na (
watatu kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero,
Dennis Londo.
Katibu
Tawala wa mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kushoto)
akimkabidhi kadi ya bima ya afya ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
Iliyoboreshwa Nelasi Nyingi , mkazi wa kata ya Mlimba , halmashauri ya
wilaya ya Kilombero wakati wa zoezi la ugawaji kadi hizo kwa
wapatao 2,100 kutoka vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba (
kushoto ) ni mkuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo na ( watatu
kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero, Dennis
Londo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya Kilombero , Dennis Londo ( kulia) akitoa
maelezo mafupi ya mapango wa kuwakatia bima ya afya wazee wasiojiweza
kwa Katibu tawala mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari ( wapili kutoka
kushoto) wakati wa zoezi la ugawaji kadi za CHF Iliyoboreshwa kwa
wazee wapatao 2,100 wa vijiji 23 vya kata saba za Tarafa ya Mlimba.
Baadhi
ya wazee wa kata saba za tarafa ya Malimba , halmashauri ya wilaya ya
Kilombero wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu tawala mkoa wa Morogoro,
Clifford Tandari ( hayupo pichani) wakati wa zoezi la ugawaji kadi za
CHF Iliyoboreshwa kwa wazee wapatao 2,100 wa vijiji 23 vya kata
saba za Tarafa ya Mlimba. ( Picha na John Nditi).