Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) pamoja na Katibu
Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia)
wakizungumza na Mbunge wa viti maalumu, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati
ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Zainabu Mwamwindi
wakiwa wameongozana na Wajumbe Kamati hiyo wakati walipotembelea jana
Jengo la Makumbusho ya Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia
ya Binadamu katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Katibu
Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (kulia)
akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga
(kushoto) wakiwa na Wajumbe Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi,
Maliasili na Utalii wakati walipotembelea jana Jengo la makumbusho ya
Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko la historia ya Binadamu katika
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii , Kemilembe
Luota ( wa kwanza kushoto) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Maj.
Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) wakiwa na baadhi ya Wajumbe wa
kamati hiyo wakiwa kwenye ‘’View Point’ kituo ambacho hutumika kuangalia
bonde la Ngorongoro kabla ya kutelemka katika Bonde hilo jana wakati
walipofanya ziara ya kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Huyu
ndiye Faru Fausta ni faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa
miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na
wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii
na Waandishi wa habari wakiji’selfie’ katika banda la Faru Fausta ambaye
ndiye faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na
anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi
kutoka kila pembe ya dunia wakati walipotembelea banda hilo kwa ajili ya
kujionea
Baadhi
ya Msururu wa Magari yaliyokuwa yamewbeba wjumbe wa kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na viongozi na watumishi wa
Wizara pamoja na wa Ngorongoro kwa ajili ya kutelemka kwenyeBonde la
Ngorongoro.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii
wakiwa katika nje ya ofisi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili
ya kuanza ziara.
Kundi
la Simba wakiwa wamepumzika walipoonekana jana wakati Kamati ya Bunge ya
Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipofanya ziara ya kutembelea
Bonde la Ngorongoro.
Bonde
la Olduvai Gorge ambako ni chimbuko la historia ya binadamu ni kivutio
cha kinachowavuta watalii wengi kutembelea eneo hilo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga( wa kwanza kushoto)
akiteta jambo na Wakurugenzi wa Wizara hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea jana
Makumbusho ya Olduvai GorgeMhifadhi
Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi akizungumza
jana kwenye kikao cha Majumuisho na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu
ya Ardhi, Maliasili na Utalii mara baada ya kukamilisha ziara ya
kutembelea Bonde la Ngorongoro na Makumbusho ya Olduvai Gorge.(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA –MALIASILI NA UTALII
Kamati
ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro kwa kazi nzuri iliyofanya ya ujenzi wa jengo la
makumbusho ya kisasa katika Bonde la Olduvai ya Gorge ambako ni chimbuko
la historia ya Binadamu.
Kamati
hiyo imesema imeridhishwa na ujenzi wa jengo hilo ambalo litawavutia
watalii na wanasayansi wabobezi wa masuala ya Malikale kutembelea
Makumbusho hiyo.
Kamati
hiyo ilibainisha kuwa Makumbusho hiyo mbali ya kutumika kuingiza pesa
kupitia watalii pia inatumika kama kielelezo na utambulisho muhimu wa
taifa katika kutangaza utamaduni wa Mtanzania ndani na nje ya nchi.
Hayo
yalisemwa jana na Kamati hiyo wakati ilipofanya ziara ya kutembelea
Ngorongoro Crater na Makumbusho ya Olduvai Gorge katika Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo. Kemilembe Luota ameipongeza Serikali pamoja na
wataalamu kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuhakikisha kuwa eneo la
Olduvai Gorge linakuwa kivutio bora kwa ajili ya historia ya nchi na
kivutio kikubwa cha Utalii duniani.
‘’
Sisi kama Kamati tunaipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa
kuyafanyia kazi mapendekezo yote tuliyoyatoa kwa mara ya kwanza
tulipokuja kwa vile tumeona kazi nzuri imefanyika.’’
Katika
hatua nyingine, Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa wananchi kutembelea
makumbusho hiyo kwa vile idadi ya watalii wa ndani aliyokutana nayo sio
ya kuridhisha.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema makumbusho hiyo
inatoa ushahidi dhahiri kuwa hata wazungu, mababu zao walitoka Afrika.
Mjumbe
wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema
Makumbusho hiyo hadi hapo ilipofikia imeboreshwa kwa kiwango cha hali ya
juu hata hivyo ameitaka Wizara ihakikishe inaitangaza ipasavyo ili
watalii wengi zaidi wazidi kutembelea.
Awali,
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, FredyManongi amesema tangu kuzinduliwa
kwa makumbusho hiyo kwa wiki moja imekuwa ikipokea zaidi ya watalii
wapatao 40000 hali inayopekelea kuwa ni miongoni mwa Makumbusho
inayofanya vizuri zaidi barani Afrika