Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiwasili katika Gereza la
Mahabusu Keko jijini Dar es salaam katika ziara yake ya kikazi kukagua
gereza hilo leo Januari 28, 2018 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki
ya Sheria hapa nchini. Jeshi la Magereza ni moja ya wadau muhimu katika
sekta ya Sheria hapa nchini. Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa
Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah
alipowasili katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo ikiwa ni
sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Wengine ni Maafisa
Waandamizi wa Jeshi hilo. Mkuu
wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi
Abdallah akitoa taarifa fupi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini Dkt. Juma Malewa kabla ya kumkaribisha kuongea na Mahabusu wa
Gereza Keko(hawapo pichani). Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongea na Mahabusu wa
Gereza Keko(awapo pichani) leo Januari 28, 2018 alipotembelea gereza
hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini.Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimsikiliza Mahabusu
ambaye ni raia wa kigeni mara baada ya kuongea na Mahabusu wa Gereza
Keko.
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini Dkt. Juma Malewa akikagua jiko la gesi katika Gereza la Mahabusu
Keko. Jeshi la Magereza tayari limeanza kutekeleza maelekezo ya Serikali
ya kuachana na matumizi ya kuni kwa kutumia nishati ya gesi katika
baadhi ya magereza nchini hivyo kutunza mazingira.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la
Magereza wakiwa katika chumba Maalum, Gereza Keko ambapo chumba hicho
kitatumika katika Uendeshaji wa Mashauli mbalimbali kwa kutumia njia ya
TEHAMA. Uwepo wa mfumo huu utalipunguzia gharama Jeshi la Magereza
katika kuwasafirisha Mahabusu mahakamani na kuwarejesha magerezani.
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika Chumba Maalum ambacho
kitatumika katika uendeshaji wa mashauli kwa kutumia njia ya TEHAMA(wa
kwanza kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es
Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Noel James(wa kwanza kulia) ni
Mkuu wa Gereza Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).