SHIRIKA
la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kutoa taarifa ya kuomba radhi wateja wanaotumia
mfumo wa "e - payment" ili kuunganishiwa umeme "service
line" kwa kushindwa kupata huduma hiyo kutokana na hitilafu iliyotokea
katika mfumo huo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 30, 2017 na Kaimu Meneja Uhusiano
TANESCO, Bi. Leila Muhaji, wataalamu wa Tehama (ict) wa Shirika hilo wanaendelea
na jitihada za kurekebisha hitilafu hiyo ili kuurejesha mfumo katika hali yake
ya kawaida. “Tutaendelea kutoa taarifa zaidi na kwa mawasiliano toa taarifa
kupitia, kituo cha miito ya simu makao makuu 0222194400 na 0768 985100 tovuti:
www.tanesco.co.tz mitandao ya kijamii www.facebook/twitter.com/tanescoyetu.”
Amesema Bi. Leila na kuongeza uongozi wa
Shirika hilo unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
|
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »