JAFFO ATAKA DODOMA IWE (FRUITS CITY) MJI WA MATUNDA

April 20, 2018


Na Mahmoud Ahmad Dodoma

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo amewataka watendaji waliochini yake kuhakikisha wanahimiza wananchi kupanda miti ya matunda ndani ya mkoa wa Dodoma sanjari na Halmashauri ya manispaa ya Dodoma ili mji huo uwe mji wa matunda(Fruits City).

Kauli hiyo ameitoa mwanzo mwa wiki kwenye Chuo cha Serikali za mitaa Hombolo wakati akiongea na wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho wakati akizindua mnara uliopewa jina la Magufuli Square kuenzi utendaji wa mh.Rais.

Amesema kuwa anataka kuona upatikana wa matunda kwenye mji wa Dodoma kuanzia kwenye Bara bara zote za mji huo wanapanda mitii ya matunda ili kuweza kuwa na mji wenye urahisi wa upaitikanaji wa matunda.

“Nataka mtu akiwa nahamu na matunda wakati anatembea anaweza kuyapata popote ndani ya mji huu tena kwa urahisi kuliko kutembea umbali mrefu kutafuta ukwaju au maembe” alisisitiza Jaffo.

Akizungumzia mnara huo aliozindua mh. Jaffo alisema kuwa lengo lake ni kuhamasisha watumishi wa umma kujua wajibu wao katika utumishi wao na kujitathmini katika uwajibikaji wao wakutoa huduma bora kwa wananchi

Amesema kufanyakazi kwa bidii ndio msingi katika maisha yao ya utumishi na kujali hali za wananchi wanyonge wa taifa hili kama alivyo mh. Raisi dkta John Magufuli yeye amejipambanua katika kuwajali wanyonge wa nchi hii na sisi tujitazame kama tumefanana naye katika majukumu yetu ya kila siku.

Akautaka uongozi wa chuo hicho na wanafunzi kuanza kuishi kwa mitazamo ya kuwatumikia wananchi wanyonge kwa maslahi mapana ya kuweka mbele uzalendo kwa nchi yao ilikulipeleka taifa mbele kwenye mafanikio sahihi ya uchumi wa kati.

Amekizungumzia kikundi cha ngoma kilichotumbuiza katika Hafla hiyo kwa kuutaka uongozi wa chuo hicho kuweka mikakati ya kukisaidia kuweza kuwa na miradi ya kuwainua katika kufikia kuweza kurekodi Albamu yao na kuwa na mradi wa kuku ili kuwa mfano na Alama ya chuo hicho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »