Imeelezwa kuwa, miradi ya ufungaji wa mifumo ya umeme jua ipatayo 20,000 ipo mbioni kuanza katika maeneo ya visiwani na makazi yaliyo vijijini ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Nishati na taasisi zake kilichoongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko jijini Dodoma hivi karibuni.
"Mradi huu unahusisha kufunga na kusambaza mifumo itakayozalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua katika makazi yaliyo vijijini ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa hasa visiwani kwa kufunga mifumo ipatayo 20,000 ndani ya miaka mitatu, " Amesema Mhandisi. Saidy
EmoticonEmoticon