Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akijaribu kukata nyama kwa
kutumia mashine ya kisasa alipotembelea ranchi ya Ruvu hivi karibuni.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina
(mwenye miwani) akiwa na viongozi wa ranchi
ya mifugo nchini akionyeshwa mbuzi wanaofugwa katika ranchi ya Ruvu
alipotembelea ranchi hiyo hivi karibuni
Jengo
la machinjio ya kisasa lililopo katika eneo la ranchi ya Ruvu ambalo Waziri wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina amewaagiza Watendaji kuhakikisha
linakamilika ifikapo Desemba 2018
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani) akihakiki taarifa za
ununuzi wa dawa za mifugo alipotembelea ranchi ya mifugo ya Ruvu hivi karibuni.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye miwani katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na watumishi wa ranchi ya Ruvu na watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi alipotembelea ranchi hiyo
jana
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mh. Luhaga J. Mpina ameagiza
machinjio ya kisasa ya Ruvu yaliyotelekezwa kwa muda mrefu kujengwa na kukamillika
ifikapo Desemba, 2018.
Maagizo hayo ameyatoa jana katika ranchi ya Ruvu, alipokuwa
katika ziara ya kutembelea baadhi ranchi za mifugo nchini, ambapo amesema ni
muhimu machinjio hayo ya ya kisasa yakamilike ili Tanzania ianze kuuza mazao
yatokanayo na mifugo katika masoko ya kimataifa.
Ametoa siku tatu kwa Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi
kumpelekea mpango kazi unaoainisha namna
ya kukamilisha ujenzi wa machinjio hiyo ya kisasa ambayo baada ya kukamilika itakuwa machinjio kubwa
kuliko zote nchini.
Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya tatu katika bara la Afrika
kwa kuwa na uwingi wa mifugo hivyo hakuna sababu ya kushindwa kuongoza
katika soko la mazao ya mifugo katika
masoko ya duniani.
Aidha, Waziri Mpina
amesema kukamilika kwa machinjio
hayo kutasaidia kupunguza usumbufu kwa
wafanyabiashara wa mifugo ambao wote nawapeleka mifugo yao Dar es Salaam hali ambayo inaongeza uharibifu wa
mazingira kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Waziri Mpina amemuagiza Mtendaji Mkuu
wa Ranchi za taifa kuhakikisha kuwa kunatafutwa fedha kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora za mifugo na kuongeza idadi ya
mifugo kulingana na uwezo wa eneo la ranchi ya Ruvu lenye ukubwa wa hekta
44,000 ambapo hivi sasa eneo hilo la ranchi ya Ruvu lina mifugo ipatayo 1530
wakati uwezo wa ni kuwa na mifugo kuanzia 12000 hadi 22000.
Alisisitiza kwamba maboresho hayo lazima yafanyike ifikapo
Desemba , 2018 ambapo ifikapo Juni 2018
tathimini ya awali itafanyika kuona ni kwa namna gani agizo hilo limetekelezwa.
“Tunataka wananchi wapate sehemu ya kujifunza,ranchi ya Ruvu
iwe sehemu ya kupata mbegu bora. Siwezi kuwa Waziri wa Mifugo wakati shamba
langu halina mifugo” alisisitiza Mpina.
Waziri aliongeza kuwa na mfumo wa kisasa wa kufuga mifugo kitaalamu badala ya mfumo wa sasa ambapo mifugo inafugwa
kwa muda mrefu.
EmoticonEmoticon