Jumanne ya Kutoa-Zaidi ya Million 20 zapatikana Kusaidia watoto wenye matatizo ya Vichwa vikubwa na Mgongo wazi

November 29, 2017
Zaidi ya milioni 20 zimetolewa na wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali hapa  nchini ikiwa ni mchango wa kusaidia matibabu na kununua vifaa tiba kwa ajili ya  watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.
Ikiwa Jana ni Jumanne ya kutoa (GIVING TUESDAY) kote duniani na Taasisi ya Foundation for Civil Society iliadhimisha kwa kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapatia vitu hivyo,huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni changia, okoa maisha.

Akikabidhi misaada hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society Bw. Francis Kiwanga alisema kuwa wafanya kazi wa Taasisi hiyo huwa wanatenga asilimia moja kwa kila mtumishi katika mshahara wake kwa ajili ya kurudisha fadhila na asante kwa jamii.
Aliendelea kwa kusema kuwa wao kama waanzilishi wa kampeni hiyo walichanga na kufikisha million sita, ila michango mingi ilitoka kwa wananchi na taasisi zilizoguswa na tatizo hilo hivyo kuona haja ya kuwasaidia watoto hao.

Aidha mkurugenzi huyo alisema kuwa msaada huo utalenga watoto 100 waliopo katika camp hizo kwa kufanyiwa upasuaji na mambo mengine madogo madogo yatakayohitajika katika zoezi hilo.

Lakini pia taasisi ya Foundation For Civil Society ikishirikiana na wadau wake wameweza kutoa kadi za bima ya afya za NHIF 100 ambazo zimegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 5 kuwasaidia watoto hao kwa matibabu hayo na mengineyo.

Aidha Mkurugenzi huyo aliwasihi  watanzania kujitolea kuwasaidia wenzetu ambao hawajiwezi na wanaohitaji michango yetu kwani kutoa ni moyo na kadiri unavyotoa ndivyo unavyobadirikiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kitengo cha mifupa MOI Dr. Respicious Boniface alisema kuwa watoto hao wakipatiwa matibabu mapema wanaweza kuwa sawa kama watoto wengine, lakini kinachofanya wazazi washindwe ni gharama za matibabu.

Daktari huyo alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili wao kama wauguzi ni uchache wa vyumba vya upasuaji kwani vyumba vilivyopo havitoshi kwa kufanyia zoezi hilo ambapo amesema kuwa kwa siku wanawafanyia upasuaji zaidi ya wagonjwa 30.

Aidha Daktari huyo aliwapongeza shirika la  Foundation for Civil Society kwa kuamua kuwasaidia watoto hao ambao wanapata tabu kwa matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi na asilimia kubwa wazazi wao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akizungumza katika maadhimisho ya Jumanne ya kutoa maarufu kama GIVING TUESDAY yaliyofanyika kitengo cha MOI Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akitoa neno la shukrani kwa wadau waliotoa msaada katika taasisi hiyo kwa kusaidia watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi Katika Taasisi ya mifupa MOI Jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akimkabidhi zawadi ya cheti Mwenyekiti wa UN chapter UDSM Bi. Faith Lawrance Katika shughuuli hiyo.



Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface akimkabidhi zawadi ya cheti Bi. Adella January Msofe katika maadhimisho ya siku ya kutoa duniani maarufu kama GIVING TUESDAY Muhimbili Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga akimkabidhi hundi ya shilingi milioni nane Mkurugenzi  Mtendaji wa taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dr. Respicious Boniface kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.


Baadhi ya wazazi na wageni walioudhuria hafla hiyo ya kutolewa kwa msaada wa kusaidia matibabu kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi jijini Dar es salaam.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »