Greyson Mwase na Asteria Muhozya.
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki ameeleza vipaumbele vyake katika Wizara
kuwa ni pamoja na udhibiti wa utoroshaji wa madini nchini, maslahi kwa
wafanyakazi huku akiwataka watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na weledi
wa hali ya juu.
Kairuki
ameyasema hayo mapema leo tarehe 10 Oktoba, 2017 jijini Dar es Salaam
alipozungumza na watumishi wa Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake,
waliopo Dar es Salaam na Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Lengo La kikao
hicho lilikuwa ni kufahamiana na kupanga mikakati ya kushirikiana ili
kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji
wa Uchumi wa nchi.
Taasisi
zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini
Dodoma (MRI) pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini
na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji
(TEITI).
Amesema
kuwa Sekta ya Madini inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa wa ukuaji wa
uchumi wa nchi na kuwataka wataalam wa madini kubuni mbinu za ukusanyaji
wa maduhuli pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye uchimbaji
madini.
Katika
hatua nyingine aliwataka wataalam hao kubuni mikakati ya kuzuia
utoroshaji wa madini nchini ili nchi ipate mapato stahiki.Amewataka
watumishi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwa wabunifu ili sekta
hiyo iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
Naye
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewakumbusha watumishi
kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara ikiwemo kufanya kazi kwa tija ili
hatimaye sekta ya madini iweze kuchangia katika uchumi wa nchi kwa kuwa
mchango wa sekta husika bado ni kidogo.
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) akitoa maelekezo kwa watumishi
wa Wizara ya Madini na Taasisi zake (hawapo pichani) Kulia ni Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.
Kaimu
Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James
Mdoe (kushoto mbele) pamoja na watendaji wengine wa Wizara wakifuatilia
maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.
(hayupo pichani).
Sehemu ya watendaji wa Wizara ya Madini wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akifafanua jambo katika
kikao hicho. Kushoto ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.
Kamishna
wa Madini Nchini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia mbele) akieleza
majukumu ya Wizara ya Madini kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki na
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hawapo pichani)
Sehemu
ya watumishi wa Wizara ya Madini, Makao Makuu Dodoma wakifuatilia
maelekezo kutoka kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo pichani)
kwa njia ya video conference.
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) na Naibu Waziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo(kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na
Kaimu Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa
James Mdoe (hayupo pichani)
EmoticonEmoticon