TAASISI YA GOODWILL&HUMANITY FOUNDATION YALAANI NDOA ZA JINSIA MOJA

April 20, 2023


MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akizungumza wakati wa hafla ya Iftari aliyoaiandaa kwenye Kituo hicho

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Mwanaidi ambaye ni Afisa Tarafa wa Ngamiani Kati akizungumza

Msimamizi wa Casa Della Giaio Sista Consolata Mgumba akizungumza wakati wa halfa hiyo ambapo aliiasa jamii ipunguze ubinafsi na kurudisha moyo wa kujali kuwaangalia wengine na kuwajaali.






MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari

MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari

MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari






Na Oscar Assenga,TANGA

MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi amesema kwamba taasisi hiyo inalaani vikali ndoa ya jinsia moja ikiwemo vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wakina mama.

Muhdar alitoa kauli hiyo wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kueleza namna walivyopingana na vitendo hivyo na kuitaka jamii kutokubali kushiriki kwenye mambo hayo

Alisema kwamba wanataka kuiambia dunia kwamba taasisi hiyo ina laani ndoa za jinsia moja na inakemea vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikifanywa kwa watoto na wakina mama kwa kuitaka jamii kubadilika na kuachana navyo.

“Taasisi hii tuna laani ndoa za jinsia moja na hatuviungi mkono kwani sisi ni moja ya huduma tunazotoa ni kuhifadhi watoto waliopotea na waliofanyiwa ukatili na Tuna Afisa Ustawi maalumu wa kuambatana na maafisa wa serikali kuwapelekea mahakamani wanaowafanyia ukatili watoto wenye kesi zinayowakandamizi watoto tunaokuwa nao kwenye makazi yetu”Alisema

“Kwani tumekuwa tukipokea watoto wamekatwa masikio,watoto wamekatwa mikono,wamemiminiwa nailoni iliyochomwa moto,waliocopmwa midomoni ,waliovuliwa nguo na kumiminiwa nailioni na kuwababua ngozi hizo ni changamoto kubwa wanazokumbana nazo watoto”Alisema

Aidha alisema kwamba wao wanaungana na kauli ya Serikali ya kukataa ukatili dhidi ya watoto na leo wametoka kuiambia dunia ukatili dhidi ya watoto haiwezekani ikiwemo ndoa ya jinsia moja haikubaliki na hawapo tayari kuwa na taifa ambalo limejaa mashoga na lenye wanawake wasagaji .

“Tumewaita kuja kufuturu pamoja ni kuthamini mchango wenu kwenye taasisi hii ambayo imeundwa kwa lengo la kusaidia mayatima,wazee, walemavu na makundi yasiyojiweza”Alisema

Awali akizungumza Msimamizi wa Casa Della Giaio Sista Consolata Mgumba aiasa jamii ipunguze ubinafsi na kurudisha moyo wa kujali kuwaangalia wengine na kuwajaali.

“Tujiulize watoto yatima kwanini zamani hayakuwepo familia tuacha kukimbia maajukumu yetu na tuwapeleka watoto kwenye vituo hivyo ikiwa hakuna msaada wowte kwenye jamii kwani wana jamii zao “Alisema

Aidha aliwataka wazingatie maadili huku akieleza kwamba mambo ya ushoga inatokana na wakina mama kutokutaka kuishi na wanaume badala yake wanalea watoto pekee yao na hivyo kuwajenga watoto kwenye mitazamo isiyosawa hivyo wao wataendelea kulipigia kelele jambo hilo.

Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa iftari hiyo Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Mwanaidi ambaye ni Afisa Tarafa wa Ngamiani Kati alitoa wito kwa wazazi na walezi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili kwenye jamii zao kutokana na kwamba hali sio nzui

Mwanaidi alisema kwamba wazazi watoe taarifa na wae na kauli kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili kwenye jamii

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »