Mkurugenzi
wa uendeshaji na Teknohama kutoka makao makuu ya benki ya Posta (TPB)
Jema Msuya (wa pili kutoka kushoto) akikabidhi mashuka na vyandarua kwa
afisa takwimu wa halmashauri ya mji wa Kahama Flora Sangiwa ambaye
alimwakilisha mkurugenzi.
*****
Takriban
wagonjwa elfu 24 hadi elfu 30 wanapokelewa kila mwezi katika hospitali
ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga idadi ambayo inatajwa kuwa ni kubwa
ukilinganisha na miundombinu ya hospitali hiyo.
Hayo
yamesemwa leo na Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dr. Fredrick Malunde
wakati akipokea msaada wa mashuka 100 na vyandarua 50 vyenye thamani ya
shilingi milioni mbili vilivyotolewa na Benki ya TPB.
Amesema kutokana na wingi wa wagonjwa wadau wanapaswa kuguswa kutoa misaada ya vifaa ili kukabiliana na changamoto hizo.
Naye
Mkurugenzi Uendeshaji na Teknohama kutoka makao makuu ya Bank ya TPB
Jema Msuya amesema Benki hiyo itaendelea kusaidia kuchangia miradi ya
maendeleo katika sekta mbalimbali huku akiwaomba wadau wengine
wajitokeze kusaidia sekta za afya.
Afisa
Takwimu wa Halmashauri yam Mji wa Kahama, Flora Sangiwa ambaye
amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo amesema
halmashauri hiyo itaendelea kuthamani michango ya wadau wa maendeleo na
kuipongeza benki ya TPB kwa msaada huo.
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakisomba vyandarua na mashuka mara baada ya kufika katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Afisa
mawasiliano wa Benki ya TPB Moves Moses akiwaonyesha waandishi wa habari
ubora wa vyandarua walivyovitoa katika hospitali hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakiteta jambo muda mchache kabla ya kuanza kwa zoezi la ugawaji wa mashuka na vyandarua.
Mganga
mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Kahama Fredrick Malunde akiteta jambo
na meneja wa tawi la TPB Kahama wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo.
Baadhi wa
wahudumu wa afya katika hospitali ya wilaya ya kahama wakiwa katika
eneo la tukio kushuhudia utolewaji wa msaada huo wa mashuka na
vyandarua.
Waandishi
wa habari na baadhi ya viongozi wa hospitali ya wilaya ya Kahama na
wafanyakazi wa TPB wakifuatilia zoezi la utolewaji wa vifaa hivyo.
Mganga
mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Fredrick Malunde aliyesimama
akitoa tathmini ya hali ya hospitali kuhusu upungufu wa mashuka na
vyandarua katika hospitali hiyo.
Baadhi ya wahudumu wa afya wakifuatilia zoezi la utolewaji wa vifaa hivyo katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Mganga
mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dr Lucas David aliyesimaam akitoa
neno la shukrani kwa bank ya tpb katika zoezi la kupokea vifaa hivyo.
Afisa
takwimu wa halmashauri ya mji wa Kahama Frola Sangiwa aliyemwakilisha
mkurugenzi wa mji akitoa neno kwa niaba ya halmashauri.
Mkurugenzi
wa uendeshaji na Teknohama kutoka makao makuu ya Benki ya TPB Jema
Msuya akitoa neno wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo.
Afisa
takwimu wa halmashauri ya mji wa Kahama Frola Sangiwa aliyemwakilisha
mkurugenzi wa mji akimkabidhi bahasha ya neno la shukrani Jema Msuya
kutoak Benki ya TPB
Picha pamoja baada ya makabidhiano ya vifaa hivyo katika hospitali hiyo.
Mkurugenzi
wa uendeshaji na Teknohama kutoka makao makuu ya Benki ya TPB Jema
Msuya akiwa na mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Fredrick Malunde
wakimfunika mgonjwa na shuka jipya lililotolewa na benki ya TPB
Zoezi la kuwafunika wagonjwa likiendelea katika wodi ya wanawake.
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakitoka katika hospitali hiyo
EmoticonEmoticon